Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

AZAM YATOA ADHABU KOMBE LA UHAI


Wachezaji wa Azam Academy wakiwa na Abedi Pele alipotembelea Azam Complex. Leo wameua 2-0.

Na Prince Akbar wa Bin Zubeiry
AZAM FC imeanza vema michuano ya Kombe la Uhai, inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuilaza Mgambo Shooting mabao 2-0 jioni ya leo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Shukrani kwao, Jamil Mchaulu ‘Balotelli’ na Reyna Mgugingila, wafungaji wa mabao hayo leo katika mchezo huo wa Kundi B.
Katika mechi za asubuhi, Coastal Union ya Tanga nayo ilianza vizuri baada ya kuifunga Tanzania Prisons mabao 2-1, mchezo wa Kundi A uliopigwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Coastal Union ilimaliza kipindi cha kwanza ikiwa tayari imepachika mabao hayo yaliyofungwa dakika ya 24 na 33 kupitia kwa Ramadhan Same na Yusuf Chuma.
Tanzania Prisons ambayo itacheza mechi yake pili kesho jioni (Desemba 12 mwaka huu) Uwanja wa Azam ulioko Chamazi dhidi ya JKT Ruvu ilipata bao lake dakika moja kabla ya filimbi ya mwisho. Mechi nyingine ya asubuhi, African Lyon iliichapa mabao 4-0 Polisi Moro.
Mechi nyingine za kesho ni Toto Africans dhidi ya Coastal Union itakayochezwa saa 2 asubuhi Uwanja wa Azam. Katika kundi B, Simba na African Lyon zitaoneshana kazi asubuhi Uwanja wa Karume wakati Azam na Polisi Morogoro zitacheza saa 10 jioni kwenye uwanja huo huo.
Kundi C kesho ni Kagera Sugar vs Oljoro JKT saa 2 asubuhi Uwanja wa Karume, na Yanga na Ruvu Shooting zitaumana saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Azam.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top