* Sasa anunuliwa kwa milioni
240 na kuweka rekodi
* Simba, Azam zalamba Milioni 80 kila moja, Ngassa naye alamba mil 80 na
mshahara mnono.
Klabu ya El Mereikh ya Sudan imetoa dola 100,000 (shs 160 million)
kuzilipa klabu za Azam FC na Simba SC ili kuondoa mgogoro wa usajili wa
mchezaji Mrisho Ngassa.
Awali El Mereikh ililipa Dola za Kimarekani 75,000 (shs million 120) kwa
klabu ya Azam FC pekee kwa ajili ya usajili wa mchezaji huyo na kuzua mtafauku
mkubwa dhidi ya klabu ya Simba na kuamua kuweka pingamizi katika Shirikisho la
Kandanda nchini (TFF), CAF na Fifa.
Simba ilidai kuwa Ngassa ni mchezaji wao halali kutokana na ukweli kuwa
ilimnunua kwa shs milioni 25 zilizotakiwa na Azam FC na kumlipa stahiki zake
zote kwa mujibu wa mkataba huo.
Pamoja na kupata upinzani mkubwa kutoka kwa timu ya Azam FC kutokana na
ukweli kuwa Ngassa alikuwa akiichezea Simba kwa mkopo, Simba iling’ang’ania na
msimamo wake na kupeleka suala hilo mbele ya vyombo vya sheria vya TFF ili
kupata haki yake.
TFF ilishauri klabu hizo kukaa meza meza moja ili kuona kuwa wanaondoa
utata huo, jambo ambalo lilifanyika Jumatatu na Jumanne na kufikia muafaka huo
na El Mereikh kulipa fedha zaidi na kumfanya mchezaji huyo kusajiliwa kwa Dola
za Kimarekani 150,000 (Milioni 240 ukijumuishs Dola za Kimarekani 50,000
atakazolipwa Ngassa na El Mereikh) na kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa kwa
kitita hicho hapa nchini.
Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala alisema kuwa wamefarijika sana na
makubaliano hayo na wao kutoa kipingamizi cha Ngassa kwenda kufanyiwa vipimo
vya afya mjini Khartoum kabla ya kusaini mkataba wa kuichezea timu hiyo.
Mtawala alisema kuwa hayo ni matunda ya kujadili mambo katika meza moja
na wala si kwa kutimia vyombo vya habari kwani wao walijua haki yao ipo wapi.
Afisa Habari wa Azam FC, Jaffer Idd alithibitisha makubaliano hayo na kusema
uongozi wa klabu hiyo chini ya makamu mwenyekiti, Shan Christoms na Twalib
Suleiman aliyemwakilisha katibu mkuu, Nassoro Idrissa ndiyo waliofikia
makubaliano hayo.
Simba SC iliwakilishwa na Mtawala na Makamu Mwenyekiti, Geofrey Nyange
Kaburu aarufu kwa jina la Perez.“Ni faraja kwetu kufikia maamuzi haya, lengo ni
kumfanya Ngassa atomize ndoto yake katika soka na wala si vinginevyo,” alisema
Idd
THBUB YACHUNGUZA MAUAJI YA KIUNGONI, PEMBA
18 minutes ago
Post a Comment