Waziri-wa-Elimu-na-Mafunzo-ya-Ufundi-Dk.-Shukuru-Kawambwa
Na Thehabari.com,
Korogwe
BAADHI ya Wanafunzi
waliofanya mitihani wa mchujo wa kidato cha pili kuingia kidato cha tatu
Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe huenda wakazuiliwa kupewa matokeo yao kutokana
na kutokuwa na fomu namba 9 (TSM9) za uzajili katika shule
zao.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi hivi
karibuni wilayani Korogwe, na kuthibitishwa na Kaimu Ofisa Elimu Sekondari
wilaya hiyo, miongoni mwa wanafunzi ambao wataathirika na tatizo hilo ni kutoka
katika shule za sekondari Bungu,
Patema pamoja na Mfundia.
Taarifa zinaeleza
wanafunzi hao waliofanya mitihani yao ya mchujo ya kidato cha bila mapema
kuanzia Novemba 5, 2012 bila ya kuwa na TSM9 namba, hivyo walimu wakuu wa shule
husika kuamriwa wawasilishe namba za wanafunzi hao katika kituo cha kusaishia
mitihani hiyo.
Akizungumzia tatizo hilo, Kaimu Ofisa Elimu
Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya
Korogwe, Shaban Shemzighwa
alikiri kuwepo kwa tatozo hilo na kudai walipokea malalamiko toka ya baadhi ya
wanafunzi wa kidato cha pili juu ya utata wa suala la
TSM9.
Hata hivyo alisema
wanafunzi waliokuwa na utata juu ya suala la TSM9 waliruhusiwa kufanya mitihani
yao ya mchujo na baadaye walimu wakuu wa shule zao kuelekezwa
wanatakiwa kuwasilisha namba za wanafunzi hao kwenye vituo vya kusahihishia
mitihani ili waweze kutambulika.
“Taarifa za malalamiko
zilitufikia na baadhi ya Shule za Sekondari ambazo wanafunzi walikuwa na
matatizo hayo ni Bungu, Patema, Mfundia na nyinginezo, hapa nipo nje ya kituo
cha kazi hivyo ni vigumu kutaja idadi na shule zote,” alisema Shemzighwa
akizungumzia suala hilo.
Mwandishi wa habari hizi
alipojaribu kuzungumza na baadhi ya wakuu wa shule ambao shule zao limetajwa
kuwa na tatizo hilo walikwepa kuzungumzia, huku wakidai hawakuwa na tatizo hilo
kwa wanafunzi wao.
Mkuu wa shule ya
Sekondari ya Bungu, Dismas Kimweli akizungumza na mwandishi wa habari hizi
alipinga shule yake kuwa na tatizo hilo licha ya Kaimu Ofisa Elimu Sekondari
kuitaja shule hiyo pia kukumbwa na tatizo la TSM9 kwa wanafunzi wake kwenye
mitihani ya kidato cha pili iliyofanyika Novemba,
2012.
Jumla ya wanafunzi wa
kidato cha pili 442,925 walifanya mitihani ya mchujo wa kidato hicho mapema
Novemba 5, 2012 na watakaoshindwa kupata wastani wa alama 30 watachujwa na
kulazimika kurudia kidato hicho kwa mwaka unaofuata.
*Imeandaliwa na
www.thehabari.com kwa ushirikiano na
HakiElimu



Post a Comment