Ushauri huo ameutoa juzi wakati wa mahafali ya tatu ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastiani Kolowa (Sekomu) yaliyofanyika katika ukumbi mpya chuoni hapo.
Mkapa alisema kuwa wahitimu wengi kutoka vyuo vikuu huangaika kutafuta ajira na kuwashauri ni vyema wakawa wakabunifu wa ajira zitakazowaletea faida na kuendeleza jamii inayowazunguka na hatimaye taifa zima.
Alisema nyakati hizi kunaupungufu mkubwa wa ajira na si Tanzania bali katika nchi nyingine nyingi duniani .
Mkapa alisisitiza kuwa wahitimu ambao watakosa ajira wajiunge kwenye vikundi vya taaluma zao ili waendelee kujifunza na kubuni mbinu za kujikwamua kwenye matatizo yatakayo wakabili katika maisha yao ya baadaye.
Wakati huo huo Mkuu wa Chuo hicho cha Sekomu , Dk Stephan
Munga aliitaka Serikali kutafuta njia mbadala za kuweza kupanua wigo wa ajira ili vijana wanaotoka vyuo vikuu waweze kupata ajira pindi wanapo hitimu masomo yao ya juu.
Munga aliitaka Serikali kutafuta njia mbadala za kuweza kupanua wigo wa ajira ili vijana wanaotoka vyuo vikuu waweze kupata ajira pindi wanapo hitimu masomo yao ya juu.
Kwa upande mwingine Munga aliwataka wahitimu kutumia vyema elimu walioipata kama silaha katika maisha yao ili wapate heshima kwa jamii.
Hata hivyo aliwataka wahitimu wawe na lugha ya kiungwana katika jamii na kwamba wasidharau wengine kwa kuwa wao tayari wana elimu ya juu.
Hata hivyo aliwataka wahitimu wawe na lugha ya kiungwana katika jamii na kwamba wasidharau wengine kwa kuwa wao tayari wana elimu ya juu.

Post a Comment