|
Bwana Yussuf Hamad anaetuhumiwa kuzaa na bintie akitaka
kumpokonya kamera mwandishi wa gazeti la majira Rashid Mkwinda ili asimpige
picha |
|
Jamaa kuona amezidiwa akaamua kujifunika na shati lake
huku akitoa maneno makali kuwa nyie waandishi mmekosa cha kuandika mmeona hii
ndiyo habari hakuna habari nyingine? alihoji mtuhumiwa
huyo |
|
Huyoooo anatoka nje ya
mahakama |
|
Sasa anavaa kofia yake ili watu wasimtambue huku akisema
nifuateni niwaonyeshe kazi |
|
Njooni sasa huku kashika
jiwe |
|
Kuona anazidi kufuatwa akaamua kuondoka mahali hapo huku
akiwa na jiwe lake mkononi |
|
Mkazi wa Mtaa wa Mbete,Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana
Yussuf Hamad(39),anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa(16) jina lake
limehifadhiwa. akiingia mahakamani leo mbele yake ni mke wake na mtoto wake
aliyezaanae ambao sura zao
tumefunika
|
|
Akina mama wanamsindikiza kwa kumzomea mtuhumiwa
huyo
Mkazi wa Mtaa wa Mbete,Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana
Yussuf Hamad(39),anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa(15) jina lake
limehifadhiwa.
Hayo yamethibitishwa na Mama mzazi wa binti huyo Bi,
Regina Simon(35) baada ya kupata taarifa Mei 11 mwaka huu kuwa binti yake ana
ujauzito wa miezi minne,na kuamua kutoa taarifa kwa Balozi wa mtaa huo Bwana
Steven Ovaova ambaye naye alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji Bwana
Angelo Sanga.
Viongozi hao wa mtaa walimuita mtuhumiwa na ili kupata
ukweli wa tukio hilo,lakini mtuhumiwa alikanusha ingawa binti yake alithibitisha
kutendewa ukatili huo na kwamba alikuwa akitishiwa kwa mapanga kila alipokuwa
akifanya naye tendo la ndoa.
Baada ya uongozi kupata maelezo kutoka kwa binti huyo na
mzazi kukataa waliamua kuipeleka kesi hiyo Polisi,ambapo walitoa PF3
iliyomwezesha binti huyo kupelekwa kwa
daktari ambaye alithibitisha kuwa binti huyo ana
ujauzito.
Binti huyo amejifungua mtoto wa kike ambae sasa anamiezi
mitatu mtoto huyo kaletwa leo mahakamani kama ushahidi kesi hiyo imeairishwa
mapaka tarehe 12/12 mwaka huu
chanzo: Mbeya Yetu
|
on Thursday, December 6, 2012
Post a Comment