Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Balozi Kamala akatisha tamaa sarafu moja EAC



BALOZI wa Tanzania nchini Ubelgiji, Dk Diodorus Kamala amesema inahitajika zaidi ya miaka 15 kuunganisha sarafu moja kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kwa sababu inahitaji maandalizi makubwa na uchumi imara.
Akizungumza baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) kwenye Chuo Kikuu cha Mzumbe juzi, Dk Kamala alisema uchumi wa nchi wanachama wa EAC siyo imara na kwamba, hakuna nchi ambayo inaweza kutoa fedha kuokoa uchumi wa mwenzake utakapotetereka.
“Ulaya nchi nyingi zina uchumi mzuri, lakini angalia inapofika mwanachama mmoja uchumi wake umetetereka… Sasa kwa EAC nchi gani itatoa fedha zake kuokoa uchumi wa mwingine?” alihoji Dk Kamala.
Shahada yake alijikita kwenye utafiti kuhusu nafasi ya Tanzania katika biashara ya kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, lengo likiwa ni kuchambua na kubainisha nafasi yake kwenye EAC kabla na baada ya kuanzishwa kwa Umoja wa Forodha.
Akisoma muhtasari wa utafiti huo kabla ya Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Barnabas Samatta hajamtunukia shahada hiyo, Dk Romanus Dimoso alisema utafiti huo ulitumia methodolojia iitwayo Ex-post kuchunguza mwenendo, mpangilio, ukubwa na mwelekeo wa mauzo na ununuzi wa bidhaa za Tanzania kwenye EAC kabla na baada ya kuanzishwa kwa Umoja wa Forodha.
“Matokeo ya utafiti yameonyesha kwamba kuondolewa kwa vikwazo vya kodi na visivyo vya kodi kumesababisha kupungua kwa bei za bidhaa, pia kuongezeka kwa kiwango cha bidhaa zinazoagizwa na kuuzwa ndani ya EAC kama ilivyotabiriwa katika dhana elekezi ya utafiti huu,” alisema Dk Dimoso.
Pia, Dk Dimoso alisema matokeo ya utafiti huo yanaonyesha kuanzishwa kwa mfumo wa pamoja kutoza ushuru mkubwa wa forodha kwa bidhaa nyeti zinazoingizwa kutoka nje ya EAC hakukupunguza uingizaji bidhaa hizo.
“Utafiti umeonyesha hali ya biashara ya bidhaa za viwandani kisekta zinazouzwa na kununuliwa katika Umoja wa Forodha EAC zinafanana na faida linganishi inayotambulika ya Tanzania dhidi ya nchi wanachama, imeongezeka baada ya kuanzishwa kwa Umoja wa Forodha,” alisema.
Dk Dimoso alisema utafiti huo unahitimisha kwamba utekelezaji wa Itifaki ya Umoja wa Forodha umesababisha kuongezeka kwa bidhaa za Tanzania zinazouzwa EAC kama ilivyobashiriwa na nadharia ya umoja huo.
“Pia, utafiti umeonyesha punguzo la kodi kwa bidhaa za kundi B lilisababisha ongezeko kwa ununuzi wa bidhaa hizo kutoka EAC. Hata hivyo, utafiti umeonyesha kiwango kikubwa cha kodi kinachotozwa kwenye bidhaa nyeti zinazoingizwa kutoka nje hakikusaidia kupunguza uingizwaji bidhaa hizo.”
Alisema utafiti huo unaainisha masuala manne muhimu ya kuzingatiwa na watunga sera wa Tanzania; Viwanda vinavyozalisha bidhaa za kundi B vinapaswa kujipanga upya kuhimili ushindani, kutokana na kodi kubwa kwa bidhaa nyeti kutokusaidia watungasera wanatakiwa kutafuta mbinu mbadala.  Nyingine ni kutokana na bidhaa za viwandani kisekta, Tanzania inabidi ijipange vizuri kukabili ushindani ndani ya EAC.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top