Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TASJA yapata safu mpya ya viongozi




Viongozi wapya wa TASJA wakiwa katika picha ya pamoja waliokaa kulia ni Mwenyekiti mpya Greyson Mutembei na Katibu Mkuu wake Benard Lugongo wakiwa na baadhi ya wajumbe wapya wa kamati ya utendaji.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
CHAMA cha Waandishi wa habari za Sayansi nchini (TASJA), kimepata viongozi wapya watakiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Waliochaguliwa ni Pamoja na Greyson Mutembei, ambaye ni Mwenyekiti mpya, Bakari Kimwanga Makamu Mwenyekiti, Benard Lugongo Katibu Mkuu na Nasra Abdallah Mweka hazina.

Mbali mkutano huo umewachagua wajumbe wa kamati ya uttendaji ambao ni David Ramadhan, Asia Rweymamu, Gabriel Mushi, Restusta James, Jackob Nduye na Hamis Shimye.

Awali akifungua mkutano Mkuu huo wa mwaka, mgeni rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Hassan Mshinda, alisema ili nchi iweze kuendelea inahitaji wanasansi na wabuni wengi ambao wataleta maendeleo nchini.

“Tunajua TASJA kwa namna mlivyo mnaweza mkawa chachu ya maendeleo katika sekta ya Sayansi nchini, nasi kama wadau wakuu tunaamini waandishi wa habari mna mchango mkubwa katika wakuelimisha wananchi.

“Ahadi yangu kwenu TASJA kupitia COSTECH mnafika mbali sambamba na kuwaunganisha na taasisi zingine kimataifa,” alisema Dk. Mshinda Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Biashara na uwakala wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kilala Sendama, alisema kuwa hivi Maendeleo ya teknolojia za mawasiliano yamejkuwa yakichukua nafasi kubwa katika maendeleo ya Taifa.

“Kwetu TPC tumejiandaa katika kutoa huduma zatu ikiwemo EMS, Post Cargo na Inateranet ambayo imekuwa ikitumiwa na watanzania wetu nanyi TASJA ni moja ya wadau wetu,”alisema
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top