BENKI ya Barclays Tanzania
(BBT) imetangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Benki Bora kwa mwaka 2012 hapa
Tanzania. Taarifa hiyo ilitolewa jijini London, Uingereza, Alhamisi ya Novemba
29 mwaka huu wakati wa hafla ya Tuzo za Benki ya Mwaka zinazoratibiwa na
kusimamiwa na gazeti la Financial Times.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa BBT, Bwana Kihara Maina
alisema: “Lengo letu ifikapo mwaka 2015 ni kuhakikisha kila mtu anataka kuja
kwetu kwa kupitia kauli mbiu ya ‘Kaweke Pesa Benki’ (Go-to-bank). Heshima hii
kubwa kwetu imeletwa na moyo wa kujitoa wa wafanyakazi kwa kuwahudumia vyema
wateja wetu na hivyo kuyarahisisha maisha yao.”
Bw.Maina aliongeza: “Kwa
jumla Tanzania kuna benki 50 na kuchaguliwa kuwa Benki Bora nchini ni furaha
kubwa kwa wanafamiliwa wa Barclays, wateja na wadau wote. Hii ni kwa kutambua
uwekezaji wetu mkubwa tulioufanya katika biashara ili kutoa huduma bora kwa
wateja wetu.
Tunawaahidi Watanzania
kuwa tutawekeza zaidi na kutoa huduma za kibenki zinazokubalika
duniani.”
Kwa mujibu wa jarida
lifahamikalo kama ‘The Banker Magazine’, Barclays imeshinda tuzo hiyo ya mwaka
kutokana na matumizi ya Teknolojia ya Mawasiliano kama vile uwekezaji katika
mfumo wa kazi (workflow and imaging systems), kuanzisha huduma za bure za ATM,
kuanzisha huduma za kibenki kwa njia ya mtandao, maendeleo katika biashata ndogo
ndogo na za kati (SMEs) na kuongezeka kwa faida mwaka 2010 na
2011.
Post a Comment