Na Mahmoud
Zubeiry, Kampala
ZANZIBAR
imeingia Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA
Tusker Challenge baada ya kuifunga Burundi kwa penalti 6-5 kwenye Uwanja wa
Lugogo, mjini Kampala, Uganda jioni hii kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya
dakika 90.
Kwa matokeo
hayo, Zanzibar sasa itacheza na mshindi kati ya Kenya na Malawi katika Nusu
Fainali.
Shujaa wa
Zanzibar leo alikuwa ni Abdallah Othman aliyefunga penalti ya mwisho, baada ya
kipa Mwadini Ally kupangua penalti ya Abdul Fiston wa
Burundi.
Manahodha wa
timu zote, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Zanzibar na Suleiman Ndikumana wa
Burundin walipoteza penalti zao leo.
Ndikumana
alikuwa wa kwanza kwenda kupiga na mkwaju wake ukaota mbawa na kupaa juu ya
lango, wakati wenzake waliofunga mbali na Fiston kupoteza ni Steve Nzigamasabo,
Amisi Tambwe, Chris Nduwarugira, Leopold Nkurinkiye na Gael Duhatindavyi.
Upande wa
Zanzibar Heroes, Khamis Mcha ‘Vialli’ alikwenda kufunga penalti ya kwanza ya
Zanzibar, Adeyom Saleh Mohamed akafunga ya pili, Jaku Juma akafunga ya tatu,
kabla ya Cannavaro kumpelekea mikononi mkwaju wake kipa Arthur Arakaza wa
Burundi, Samir Hajji Nuhu akafunga ya tano, Aggrey Morris akafunga ya sita na
Othman kutumbukiza nyavuni ya ushindi.
Zanzibar leo
walicheza soka ya kuvutia na kiungo Suleiman Kassim ‘Selembe’ ndiye aliyekuwa
nyota ya mchezo kutokana shughuli kubwa aliyoifanya akicheza katika dimba la
juu.
Ndikumana
leo aliwekewa ulinzi mkali na hakuwa na madhara kwa Watanzania wa upande wa pili
wa Bahari.
Mapema
katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali, Bara ilifanikiwa pia kuingia Nusu baada
ya kuilaza Rwanda mabao 2-0 kwenye Uwanja huo huo wa Lugogo mjini hapa.
Hadi
mapumziko, Stars walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na kiungo Amri
Kiemba, dakika mya 33 akiunganisha pasi ya Mwinyi Kazimoto aliyewapunguza
wachezaji wawili wa Rwanda kabla ya kutoa pasi
maridadi.
Katika mechi
hiyo iliyochezeshwa na refa Mohamed El Fadil kutoka Sudan, mshambuliaji John
Raphael Bocco ‘Adebayor’ alikuwa mwiba mchungu kwa safu ya ulinzi ya Rwanda na
aliwafanya waende kwenye vyumba vya kupumzikia wakiwa
hoi.
Katika hicho
kipindi cha kwanza, Rwanda walikosa bao la wazi dakika ya 12 baada ya krosi ya
Jean Claude Iranzi kuokolewa na beki Kevin Yondan kwa kichwa na dakika ya 19
Jean Baptiste Mugiraneza alipiga juu akiwa nje kidogo ya eneo la
hatari.
Stars pamoja
na kufunga bao hilo kipindi hicho cha kwanza, katika dakika ya 30 krosi nzuri ya
Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mrisho Ngassa na Bocco walishindwa kuiunganisha na
ikawapita wote.
Ngassa tena,
katika dakika ya 38 alipiga shuti kali kutoka wingi ya kushoto, lakini likaenda
nje sentimita chache.
Kipindi cha
pili,
Kipindi cha
pili Stars walirudi vizuri tena na kuendelea kucheza kwa kuonana, ingawa na
Rwanda nao waliendelea kucheza kwa bidii kutafuta bao la
kusawazisha.
Hata hivyo,
walikuwa ni Stars tena waliofanikiwa kupata bao la pili 53 baada ya John Bocco
kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Jean Claude Ndoli kufuatia shuti kali la Mwinyi
Kazimoto kutoka nje ya eneo la hatari.
Baada ya bao
hilo, Rwanda walionekana kupagawa, lakini hawakusahau kushambulia lango la Stars
na dakika ya 86 Dadi Birori hakujali ameotea akasukuma mpira nyavuni, lakini
refa akakataa bao hilo.
Kwa ushindi
huo, Stars sasa inasubiri mshindi kati ya Uganda na Ethiopia kesho kukutana naye
kwenye Nusu Fainali.
Stars; Juma
Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, Amri Kiemba,
Salum Abubakar/Athumani Iddi dk51, Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto, Mrisho Ngassa
na John Bocco/Shaaban Nditi dk 85.
Rwanda; Jean
Claude Ndoli, Emery Basiyenge, Ismail Nshutimayamangara/Fabrice Twagizimana
dk19, Jimmy Mbaraga/Imran Nshiyimana dk67, Charles Tibingana/Barnabe Mbuyumbyi
dk61, Michel Rusheshangoga, Jean Baptiste Mugiraneza, Haruna Niyonzima, Jean
Claude Iranzi, Dadi Birori na Tumaine Ntamuhanga.
Post a Comment