African
Barrick Gold Maendeleo Fund inazindua rasmi mpango “Nightwatch” utakaofanyika
katika Kanda ya Ziwa. Mpango huu wa NightWatch, umeandaliwa na Malaria No More
kwa kushirikiana na Mradi wa Lalela, ikiwa ni kampeni inayoshirikisha vyombo vya
habari inayolenga kuwakumbusha watu juu ya umuhimu wa kulala kwenye vyandarua
vyenye dawa ya kudumu ili kujikinga na malaria. Afrika Barrick Gold Maendeleo
Fund na Tanzania House of Talent zinaungana kwa pamoja kutekeleza mpango huu
katika unaoanzia Kanda ya Ziwa kufikia jamii zinazoendelea kuathirika na ugonjwa
huu.. Watekeliezaji mkuu katika mpango huu, Tanzania House of Talent (THT) kwa
sasa wanarusha matangazo katika televisheni ya taifa na redio kama sehemu ya
mkakati wake wa Zinduka! Malaria Haikubaliki! Katika kanda ya Ziwa mpango
unaoungwa mkono na Afrika Barrick Gold Maendeleo Fund utatumika kama chachu
katika kuimarisha kampeni hii ya kitaifa. "Tunafurahi kufanya kazi na Tanzania
House of Talent, Malaria No More na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika
kampeni hii ya kitaifa, ili kupambana na malaria ugonjwa unaoendelea kuongoza
katika kusababisha maradhi na vifo katika Afrika. Hii inadhihirisha umuhimu wa
makampuni na wananchi wote kwa ujumla kushikiana katika kutoa elimu juu ya
malaria. Kampeni hii tumelenga Kanda ya Ziwa sehemu ambayo shughuli zetu za
uchimbaji wa madini zinafanyika. " Alisema Deo Mwanyika, ABG Vice President
Corporate Affairs. Kanda ya Ziwa inakabiliwa na tatizo kubwa la malaria
ikilinganishwa na sehemu nyingine za nchi. Tanzania National Malaria Control
Program (NMCP) imesimamia jitihada za serikali na washirika wa afya kwa kutoa
zaidi ya vyandarua vyenye dawa ya kudumu milioni 26 miaka 3 iliyopita na pia
kuongeza upatikanaji wa dawa ya ukoko, uchunguzi na matibabu ya malaria. Ili
kuhakikisha kwamba mafanikio haya yanadumishwa katika kupambana na malaria, NMCP
inahimiza na kuunga mkono kampeni za mawasiliano. NightWatch inaimarisha
upatikanaji wa taarifa kuhusu malaria kwa njia mbalimbali, hivyo inawezesha
tabia za kudhibiti malaria kama vile kulala kwenye chandarua chenye dawa kila
usiku, kwenda kupata matibabu haraka kuwa tabia ya kawaida na inayozoeleka.
Programu ya Nightwatch kwa kanda ya Ziwa imeshirikisha wasanii maarufu nchini
Tanzania kama vile Diamond, Masanja Mkandamizaji, Mwasiti, Dina Marios,
Mheshimiwa Vicky Kamata (Mbunge) na Barnaba ambao watatumia nafasi yao kutoa
ujumbe nyakati za usiku kuhusu malaria kupitia vituo vya redio za jamii. "Lengo
kubwa la kampeni ni kuwahamasisha Watanzania kuchukua hatua na kujizuia wao
wenyewe na watu wengine kutoambukizwa malaria katika jamii yao. Kupitia kampeni
hii, tunatarajia kumwezesha kila mtu kuchukua hatua na kulinda wenyewe na
familia yake kutokana na malaria, " alisema Mwasiti, Balozi wa mradi wa Zinduka.
"Kampeni hii inatarajiwa kujenga harakati nchini kote, na natumaini yangu kwamba
mpango huu wa NightWatch utaongezea nguvu jitihada ambazo jamii imekua ikifanya
katika sehemu wanazoishi." Ujumbe wa Nightwatch utaanza kusikika Disemba 14,
2012 Passion FM na Kwizera FM Kwa taarifa zaidi za kampeni ya NightWatch:
http://www.malarianomore.org/what-we-do/tanzania- nightwatch
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
-
Kwa Undani5 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
Serikali yatoa kauli kuhusu Dbi ya Kariakoo9 months ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-



Post a Comment