Tanzania Bunge Sport
Club Netball imefanikiwa kuwa kileleni baada ya kuitandika timu ya muungano ya
Jumuiya na Bunge la Afrika Mashariki kwa mabao 49-9.
Katika mchezo mkali wa
mashindao ya michezo ya mabunge yanayoendelea jijini Nairobi, Kenya, timu ya
Tanzania imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuwachakaza bila huruma wenyeji
wao Kenya kwa mabao 51-25.
Mashindano haya ambayo
huandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Bunge la Afrika
Mashariki kwa lengo la kudumisha mshikamano, yanatarajiwa kufikia kilele tarehe
14 Disemba 2012.
Tayari Tanzania imeweka
kibindoni mabao 100, mtaji ambo si rahisi kfikiwa na timu nyingine zilizosalia.
Tayari Tanzania Bunge
Sports Club Football wameshajihakikishia kuingia nusu fainali baada ya kutoa
adhabu kali kwa timu za Kenya na Rwanda. Kwenye mechi yake na Kenya, Tanzania
ilijipatia mambo 5-0. Aidha kwenye mchezo wake na Rwanda Tanzania iliifunga
Rwanda mabao 6-0 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa City.
Awali Kenya Bunge Sports
Club Football ilitoka sare ya 1-1 na Afrika Mashariki katika mchezo uliopigwa
kwenye Uwanya wa Nyayo mbele ya Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Margreth
Natongo Zziwa ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo.
Aidha kwenye mchezo kati
ya Uganda na Afrika Mashariki Uganda ilijipatia mabao 2 -1, huku Rwanda
ikijipatia magoli 2-0 dhidi ya Kenya
Post a Comment