Coastal Union ya Tanga
imeanza vizuri michuano ya kuwania Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji
wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuifunga
Tanzania Prisons mabao 2-1.
Mechi hiyo ya kundi A
imechezwa leo asubuhi (Desemba 11 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume,
Dar es Salaam. Coastal Union ilimaliza kipindi cha kwanza ikiwa tayari
imepachika mabao hayo yaliyofungwa dakika ya 24 na 33 kupitia kwa Ramadhan Same
na Yusuf Chuma.
Tanzania Prisons ambayo
itacheza mechi yake pili kesho jioni (Desemba 12 mwaka huu) Uwanja wa Azam
ulioko Chamazi dhidi ya JKT Ruvu ilipata bao lake dakika moja kabla ya filimbi
ya mwisho.
Mechi nyingine za kesho
ni Toto Africans dhidi ya Coastal Union itakayochezwa saa 2 asubuhi Uwanja wa Azam.
Katika kundi B, Simba na African Lyon zitaoneshana kazi asubuhi Uwanja wa
Karume wakati Azam na Polisi Morogoro zitacheza saa 10 jioni kwenye uwanja huo
huo.
Kundi C kesho ni Kagera
Sugar vs Oljoro JKT saa 2 asubuhi Uwanja wa Karume, na Yanga na Ruvu Shooting
zitaumana saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Azam.
Post a Comment