mmoja wa wahudumu wa
hospitali ya mkoa ya Mounti Meru akiwapa maelekezo viongozi wa chama cha
mapinduzi pamoja na wanachama wa UVCCM waliotembelea hospitali hiyo kwa ajili
yakutoa misaada kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapa wa kwanza kulia ni
Katibu wa UVCCM mkoa wa Arusha Salus Kidima akifuatiwa na mwenyekiti wa UVCCM
mkoa Robson Meitinyiku
mjumbe wa baraza kuu la
UVCCM taifa toka mkoa wa Arusha Benson Mollel wa kwanza kushoto akifuatiwa na
mwenyekiti UVCCM mkoa Robson Meitinyiku wakiwa wanatoa msaada kwa mtoto Frank
aliyekuwa amelazwa hospitali ya mounti meru
Mwenyekiti wa UVCCM
Robson Meithinyiku akiwa anapeleka
msaada kwa wamama waliokuwa wamelazwa wodini
Picha juu na chini
ni wajumbe wa UVCCM pia walikuwepo katika swala zima la kugawa misaada kwa
wagonjwa walikuwa wamelazwa katika hospitali ya mounti meru
Mwenyekiti akimfariji
mtoto mara baada ya kumkabidhi msaada
Viongozi wa chama cha
mapinduzi wakiwa wanaimba wimbo wa chama kabla ya mkutano wa baraza la uvvccm
mkoa wa Arusha
Mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Arusha Onesmo Nangole akiwa anazindua rasmi mkutano wa baraza la UVCCM
uliofanyika katika hotel ya golden rose mkoani Arusha ambapo katika mkutano huo
walizungumzia mambo mengi ikiwemo kuondoa makundi yaliopo katika chama chao na
kujipanga kikamilifu katika kuimarisha chama
chao
wajumbe walikuwa
makini kusikiliza nini haswa kinazungumzwa
CHAMA Cha Mapinduzi kimesema chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA)mkoani Arusha kilitumia mbinu chafu kushinda katika
uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya daraja mbili jijini
Arusha.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Onesmo Nangole
alitaja moja ya mbinu hizo kuwa ni kuwashawishi wafuasi wake kupiga kura mapema
na kasha kuanzisha fujo ili kuwatisha wanawake na wazee kutojitokeza kupiga
kura.
Aliyasema hayo jana alipokua akifungua kikao cha
baraza maalumu la UVCCM mkoani hapo ambacho mbali na ajenda zingine kilichagua
wajumbe wa kamati ya utekelezaji na katibu hamasa wake.
Alisema kutokana na vurugu hizo walizokua
wakifanyiwa watu wa makundi hayo pindi walipokua wakitoka majumbani mwao kwenda
katika vituo vya kupigia kura vilisababisha wengi wao kurudi majumbani mwao kwa
kuhofia usalama wao.
Alisema baadhi ya watu wa makundi hayo
waliofanikiwa kupiga kura walilazimika kusindikizwa na vijana wa CCM kwenda
vituo vya kupigia kura lakini wengi walishindwa kutokana na kuchelewa
kugundulika kwa mbinu hiyo chafu kwa vyombo vya dola likiwemo jeshi la
polisi.
Kufuatia vitendo hivyo Nangole aliwataka vijana
hao kupitia jumuiya yao hiyo kujibu mapigo hayo dhidi ya vitendo hivyo vichafu
kwa wao nao kujitokeza kwenda kupiga kura mapema ili kupambana na wafuasi na
vijana wa Chadema pindi kutakapojitokeza chaguzi
zingine.
Alisema haiwezekani waoa kama vijana ambao ndiyo
jeshi la CCM na wananchi wake wakakalia kimya mambo hayo na kuhatarisha usalama
wa chama,wanachama na wananchi wao katika kipindi cha chaguzi
mbalimbali.
Nae mwenyekiti wa umoja huo mkoani hapo Robson
Meitinyiku alimuahidi Nangole kutorejea kwa vitendo hivyo chini ya uongozi wake
kwakua nao ni vijana na mbinu chafu pia wanazijua pamoja na kupambana na wafuasi
hao.
Alisema mbali na kujibu mapigo hayo pia watatumia
nafasi yao kama jeshi la chama katika kuhamasisha vijana wake,wanawake na wazee
kujitokeza mapema kupiga kura pamoja na kuwalinda ili kuwzesha chama kuendelea
kushika dola.
“mwenyekiti nikuhakikishie kwamba suala hilo
halitajirudia tena tumejipanga vyema vijana watawahi kupiga kura ili wawalinde
mama zetu na wazee wetu hayo yaliyojitokeza yatakua historia tuu”alisema
Meitinyiku.
Aidha alimuahidi mwenyekiti huyo kuwa chama cha
mapinduzi kitalirejesha jimbo la Arusha iwapo uchaguzi utarudiwa kwakua kwasasa
jumuiya yake imejipanga vyema baada ya kutambua madhara ya jimbo hilo kwenda
upinzani ikiwemo hata wao kama vijana kuporomoka
kiuchumi.
Katika kikao hicho wajumbe wa watano walichaguliwa
kuunda kamati ya utekelezaji ambapo kwa wilaya ya Arusha alichaguliwa Amina
Msangi,KaratuJackob Doday,wilaya ya Meru Titto Nassari,Arumeru Noel Severe na
Monduli Diwani Kimey huku katika nafasi ya katibu hamasa alichaguliwa kwa mara
nyingine mtoto wa mbunge wa Monduli Edward Lowassa,Fred
Lowassa














Post a Comment