Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Dk. Mohammed Gharib Bilal amesema suala la elimu kwa Waumini wa dini ya Kiislamu lipewe kipaumbele

 
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Mhe. Rais Jakaya Kikwete, kutoka kwa Kiongozi wa Umoja wa Wanazuoni, nchini Kuwait, Jasem Mohamed Alitn, baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Wanazuoni wa Bara la Afrika, ulioanza leo Desemba 15, 2012 katika ukumbi wa PTA, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
…………………………………………………………
MAKAMU wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal amesema suala la elimu kwa Waumini wa dini ya Kiislamu, linatakiwa kupewa kipaumbele kama ilivyo katika Kitabu Kitakatifu cha Qur’an na Sunnah.
Kauli hiyoaliisema jijini Dar es Salaam jana wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa pili wa Wanazuoni wa dini ya kiislamu wa Bara la Afrika uliowashirikisha na Said Arabia.
Bilal alisema jamii ya waislamu katika nchi mbalimbali barani afrika ikiwemo Tanzania wako nyuma katika suala la elimu sanjari na maarifa.
“Kutafuta elimu ni faradh kwa kila muislamu, mbaya zaidi imefika sasa waislamu wengi hawaijui dini yao vizuri, jambo ambalo ni hatari kwa sababu limesababisha mmong’onyoko wa maadili miongoni mwa jamii wakiwemo wao wennyewe”alisema Dk. Bilal.
Katika hilo, alitolea mfano wa maandiko katika aya ya 31 ya Surat Al Baqraha, yasemayo “Na tukamfundisha Adam majina ya vitu vyote”, vile vile katika amri ya kwanza kuteremshiwa Mtume Muhammad (Swalla Aliwaahu alayhi wa sallam) ni ‘IQRA’ yaani soma.
Pamoja na hayo, alisema endapo waislamu watazingatia umuhimu wa elimu ya mwongozo na maarifa katika dunia, wataweza kutatua matatizo yanayowakabili wananchi wakiwemo waislamu wenyewe hususani yakiwemo yale ya uharibifu wa maadili, uasherati, ukosefu wa ajira, unyanyasaji wa kijinsia pamoja na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU).
“Dunia tunayoishi sasa ni ya utandawazi, na hakuna jamii itakayoweza kuishi kama kisiwa, hivyo basi Wanazuoni wa Kiislamu pamoja na viongozi wengine wa dini, mnapaswa kuangalia ni jinsi gani utandawazi hautoathiri imani na maadili ya waumini, ingawa watanufaika na maendeleo ya sayansi na Teknolojia” alisisitiza Bilal.
Kadhalika alisema kuwa, licha ya waumini wengi ni waislamu na wakristo, lakini kuna haja ya kujenga maelewano mazuri baina ya wafuasi wa dini hizo, vinginevyo nchi inaweza kushuhudia migogoro ya kidini ikiendelea kutokea kama ilivyojitokeza katika nchi ya Nigeria ikiwemo Tanzania.
Aidha, alisema mkutano huo utumike kama chachu ya kutafakari matukio mbalimbali ya vurugu za kidini ambayo yametokea Tanzania kwa lengo la kuweka utaratibu mzuri wakuishi kwa kuheshimiana kati ya pande zote mbili, kwa sababu Imani si ugomvi bali inapaswa iwajenge waumini kimaadili hata kama siyo wa imani yake.
“Lengo ni kuondoa tofauti zilizopo baina ya dini zote mbili na hata zaidi, hususani kwa waislamu wanaosifika kwa kufarakana, wasiyo na elimu, wasioheshimu wengine pamoja na kutotambua nafasi ya mchango wao katika maendeleo ya nchi”alisema.
Naye Mwakilishi wa Balozi wa Saud Arabia,Mohamed Al Twalah alisema mkutano huo ambao umewahusisha wananzuoni wa ndani na nje ya nchi utawapa fursa kuyatafutia ufumbuzi yale watakayoyajadili katika mkutano huo.
“Dini ya kiislamu inahimiza kushi kwa amani na kuwalinda watu pamoja na mali zao bila kuangalia aina ya dini”.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top