Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Avigodor Lieberman, amejiuzulu baada ya kushtakiwa kwa makosa ya udanganyifu na kuvunja uaminifu.
Hatua ya kujiuzulu kwa Lieberman inaweza kuwa na athari katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika Januari mwakani.
Chama cha mrengo wa kulia cha Lieberman pamoja na kile cha Likud kinachoongozwa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, viliunda muungano wa kisiasa kuelekea uchaguzi huo.
Kura za maoni zimeonyesha kuwa huenda muungano huo ukashinda.
Hata hivyo Kiongozi huyo amekana shutuma zinazomkabili ambazo zilitolewa na Mwanasheria Mkuu na haijafahamika kama atashiriki uchaguzi mkuu Januari 22 mwaka ujao.


Post a Comment