John Bocco |
Na Mahmoud
Zubeiry wa Bin Zubeiry
AJABU na
kweli. Robert Ssentongo amepewa tuzo ya ufungaji wa Kombe la Kombe la Mataifa
ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge jana, wakati anazidiwa
mabao na washambuliaji wa Tanzania Bara, John Raphael Bocco na Mrisho Khalfan
Ngassa, ambao kila mmoja ana mabao matano.
Ssentongo
amemaliza mabao manne, lakini jana CECAFA ikampa tuzo hiyo na kuwaacha wengi
midomo wazi.
Uganda
ilitwaa Kombe la Chalenge jana kwa kuifunga Kenya mabao 2-1, ambayo yote Kenya
walijfunga jana kupitia kwa wachezaj wao Anthony Kimani na Joackins Atudo. Bao
la Kenya lilifungwa na Edwin Lavatsa.
Mbali na
Ngassa na Bocco kuongoza wakifuatiwa na Ssentongo, wengine waliokuwamo kwenye
kinyang’anyiro ni Brian Umony wa Uganda aliyemaliza na mabao matatu, sawa Khamis
Mcha ‘Vialli’ wa Zanzibar, Suleiman Ndikumana na Chris Nduwarugira wa
Burundi.
Wachezaji
wenye mabao mawili kila mmoja ni Geoffrey Kizito wa Uganda, David Ochieng, Mike
Barasa, Clifton Miheso wa Kenya na Dadi Birori wa
Rwanda.
WAFUNGAJI
CECAFA TUSKER CHALLENGE 2012
John Bocco
Tanzania 5
Mrisho
Ngassa Tanzania 5
Robert
Ssentongo Uganda 4
Brian Umony
Uganda 3
Khamis Mcha
Zanzibar 3
Suleiman
Ndikumana Burundi 3 (1
penalti)
Chris
Nduwarugira Burundi 3
Geoffrey
Kizito Uganda 2
David
Ochieng Kenya 2
Clifton
Miheso Kenya 2
Dadi Birori
Rwanda 2
Mike Barasa
Kenya 2
Post a Comment