|
Vurugu Chunya
WATU 13
akiwemo diwani wa viti maalumu kupitia Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo(Chadema) kata ya saza Benadetha Zacharia(38) wanashikiliwa na jershi
la polisi kwa kufanya vurugu zilizosababisha uharibifu wa mali ya umma yakiwemo
masanduku ya kupigia kura.
Wengine ni
katibu wa Chadema kata ya Saza wilayani Chunya Braison Mwasimba(34),John
Mponzayo(52),Seleman Tanganyika(24),Ambokile Francis(23),Amos Joseph(24),Abdul
Mwandeule(20),Christopher Mwanjayo(37), Baraka Saul(19),Musa Mnyonga(32),Essa
Pius(18),Marco Gibson(25) wote wakazi wa kata ya Saza na Paradiso Emanuel(26)
mkazi wa kijiji cha Njenjele wilayani Mbeya. Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwan
Athuman alisema kuwa mnamo desemba 8 mwaka huu majira ya saa 11:15 katika ofisi
ya afisa mtendaji wa kata ya Saza baadhi ya wananchi wakiongozwa na watuhumiwa
waliamua kujichukulia sheria mikononi na kusababisha uharibifu wa mali za umma.
Kamanda Athuman alitaja uharibifu uliofanyika kuwa ni kuvunjwa kwa kioo cha
mbele cha gari yenye namba SM 3830 Toyota Landcruiser mali ya halmashauri ya
wilaya ya Chunya,kuvunja mlango na dirisha la ofisi ya afisa mtendaji kata.
Alisema hbaada ya uharibifu huyo watuhumiwa waliingia ndani ya ofisi hiyo na
kuharibu masanduku 24 ya kupigia kura ambapo thamani ya mali zote bado
haujafahamika. Alisema chanzo cha vurugu hizo ilikuwa kushinikiza kuzuia
kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya mwenyekiti wa kijiji na
vitongoji uliokuwa ufanyike siku ya jumapili. Kufuatia vurugu hizo uchaguzi huo
ililazimu kusogezwa mbele siku moja na kufanyika jana(Disemba 10) huktaratibu za
kisheria zikiendelea ikiwemo kufikishwa jana mahakamani katioka mahakama ya
wilaya ya Chumnuya watuhumiwa 12 na kusomewa mashitaka. Ukiachilia mbali shitaka
la uharibifu wa mali za umma linalowakabili washitakiwa wote mahakamani hapo
washitakiwa Amos Joseph,Braison Mwasimba na Paradiso Emanuel wanakabiliwa na
shitaka jingine la unyang’anyi. Alisema washitakiwa hao walifanya unyang’anyi wa
fedha kiasi cha shilingi 2,150,000 zilizokuwa sehemu ya gharama za uchaguzi,simu
ya kiganjani na saa ya mkononi
|
on Tuesday, December 11, 2012
Post a Comment