KAMPUNI ya Bia Tanzania Breweries Limited (TBL),
imeshinda kesi inayohusisha malipo ya Sh25 bilioni dhidi ya Kampuni ya
Serengeti Breweries Limited (SBL) katika hukumu iliyotolewa na Baraza la
Ushindani nchini (FCT).
Tume ya Ushindani nchini, mwaka 2010 iliitoza faini
ya asilimia tano ya mauzo TBL, kwa kujihusisha na tabia kinzani za ushindani wa
biashara dhidi ya (SBL), asilimia hiyo inafikia takriban Sh25
bilioni.
Kutokana na uamuzi huo, TBL kupitia mawakili wake
ambao ni Dk Ringo Tenga na Fayaz Bhojan walikata
rufani.
Katika rufani hiyo, mawakili hao wa TBL
waliwasilisha hoja mbalimbali, ikiwamo ya FCC haikuundwa ipasavyo kwa mujibu
wa sheria na kwamba mwenyekiti wake, Nikubuka Shimwela hakuteuliwa kama
inavyostahili.
Mawakili hao waliendelea kudai kuwa, Mwenyekiti huyo
aliteuliwa na Waziri wa Biashara siyo Rais wa nchi kama sheria ya ushindani
inavyoelekeza, hivyo kufanya uamuzi uliotolewa kuwa batili na unastahili
kufutwa.
Licha ya hoja hizo, mawakili hao wa TBL pia walidai
kuwa, Mkurugenzi huyo wa FCC naye hakuteuliwa
kihalali.
Jopo la watu watatu, lililoongozwa na Jaji wa
Mahakama Kuu, Razia Sheikh lilisikiliza rufani na kukubaliana kuwa FCC kwa
kipindi hicho haikuwa imeundwa kwa mujibu wa sheria, hivyo uamuzi wa TBL kutoa
faini hiyo haukuwa halali.
Post a Comment