Rais wa Venezuela, Hugo Chavez ambaye anasumbuliwa na maradhi ya saratani, amekabidhi baadhi ya majukumu ya kiuchumi kwa makamu wake Nikolas Maduro.
Kwa mujibu wa kanuni iliyotiwa saini na rais Chavez na kuchapishwa na gazeti la serikali, Maduro atakuwa na mamlaka ya kuchukua baadhi ya maamuzi juu ya masuala yanayohusu bajeti.
Kanuni hiyo ilitiwa saini mapema mwezi huu, siku moja kabla ya Chavez kuelekea nchini Cuba, ambako amefanyiwa upasuaji katika juhudi zake za kupambana na ugonjwa wa saratani.
Hata hivyo hakuna taarifa rasmi juu ya aina ya saratani aliyonayo rasi Chavez, lakini hali ya afya yake inayozidi kudorora imeleta mashaka juu ya mustakabali wa vuguvugu lake la mrengo wa kushoto.
Chavez mwenye umri wa miaka 58 amekuwa madarakani tangu mwaka 1999.