MUUNGANO wa Makanisa nchini
unatarajia kufanya Mkesha wa kuliombea Taifa ili amani na utulivu uliopo uweze
kudumu, ambao unatarajiwa kufanyika Desemba 31 mwaka huu kwenye viwanja vya
Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Godfrey
Malassy , alisema mkesha huo umekuwa ukifanyika kila Desemba 31 ya kila mwaka,
kuukaribisha mwaka mpya.
Alisema lengo la mkesha huo
ni kuliombea Taifa hilo mungu, ili aweze kuliponya na kulinusuru na majanga
mbalimbali, na kudumisha amani miongoni mwa jamii yote
nchini.
Malassy aliongeza kuwa
Taifa kwa sasa linapita katika kipindi kigumu hususani kuanzia uelewa, uchumi,
na katika masuala ya usalama wa raia wa ndani na nje ya nchi ambapo kuna baadhi
ya watu wameanza kuichezea amani kwa kusababisha vurugu kwa kvisingizio vya
dini.
Pia alisema kuwa Watanzania
wanapaswa kudumisha amani na utulivu kwani hiyo ni tunu ambaayo wamepatiwa na
mungu hivyo haipaswi kuchezewa na watu wachache wasio na nia
njema.
“Mkesha wa dua hilo,
utafanyika Desemba 31 mwaka huu kuanzia saa 2:00 usiku hadi asubuhi katika
viwanja vya Taifa Dar es Salaam, na tunatarajia Rais Jakaya Kikwete atakuwa
mmoja wa wageni wetu waalikwa” alisema Malassy.
Malassy alibainisha kuwa
mkesha huo wa maombezi utashirikisha mikoa zaidi ya 16 ya Tanzania Bra na
Visiwani, ambapo utakuwa na lengo la kuwaleta Watanzania kuliombea Taifa kwa
ajili ya kudumisha amani, umoja na mshikamano
visitetereke.
Post a Comment