Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar,Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar,(ZEC) Khatib Mwinyichande,akiongoza ujumbe wa Tume hiyo walipofika Ikulu Mjini Zanzibar,Kumuaga Rais kwa kumaliza muda wa kazi wa Tume hiyo jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar,Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea Ripoti ya Tume ya Uchaguz Zanzibar,(ZEC) kutoka kwa Mwenyekiti wake KhatibMwinyichande,alipoongoza ujumbe wa Tume hiyo walipofika Ikulu Mjini Zanzibar,Kumuaga Rais kwa kumaliza muda wa kazi wa Tume hiyo jana.
Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Ndugu Khatib Mwinchandeakimkabidhi Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ripoti ya Utumishi wa miaka Mitano wa
tume hiyo inayomaliza muda wake tarehe 1/1/2013.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wajumbe na
Makamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar wanao maliza muda wake tarehe 1/1/2013
wakiongozwa na mwenyekiti wao Nd. Khatib Mwinchande
Joto
la Uchaguzi miongoni mwa Viongozi wa vyama vya siasa sambamba na wanachama
pamoja na wapenzi wa vyama vya siasa litapungua au kuondoka kabisa endapo Tume
ya Uchaguzi itaendelea kuwa karibu na washirika wake.
Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar { ZEC } Ndugu Khatibu Mwinchande alisema hayo wakati yeye na
wajumbe wa Tume hiyo walipokuwa wakimuaga rasmiMakamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakikaribia kumaliza muda wao wa utumishi wa miaka
mitano unaomalizika Januari Mosi 2013.
Ndugu Khatib Mwinchande
ambae katika mazungumzo hayo akimkabidhi Balozi Seif Ripoti kamili ya Utumishi
wao wa Miaka Mitano alisema ukaribu wa Tume ya Uchaguzi kwa washirika wake ndio
njia pekee ya kuondosha malalamiko au dhana potovu ya wadau hao dhidi ya Tume
hiyo.
“ Ni mara ya kwanza
katika Historia ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kutoa fursakwa Vyama vya Siasa
kupatiwa fursa ya kulikaguwa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Hii ni ishara kwa
Tume hii kuwa karibu na wadau wake ili kupunguza joto la Uchaguzi”. Alifafanua
Ndugu Khatib Mwinchande.
Mwenyekiti huyo wa Tume
ya Uchaguzi Zanzibar Nd. Mwinchande alifahamisha kwamba daftari la wapiga kura
litaendelea kuwa la kudumu katika dhana ya kuimarisha Demokrasia licha ya
changamoto zilizopo za ukosefu wa fedha kwa ajili ya kuendeleza zoezi
hilo.
Alisema harakati za
kimaisha zinazoendelea kukuwa kila siku zinachangia kulifanya daftari hilo kuwa
la kudumu kutokana na ongezeko la idadi ya watu sambamba na baadhi ya wananchi
kuhama sehemu moja kwenda nyengine.
Akizungumzia uhusiano wa
Kitaifa na Kimataifa Ndugu Mwinchande alisema Tume ya Uchaguzi Zanzibar
imefanikiwa kuoneza ushirikiano wa karibu kati yake na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Tanzania { NEC } sambamba na Tume za Kimataifa za Nchi za Sadc na zile za Umoja
wa Afrika { AU }.
Alisema hatua hiyo
imeijengea uwezo zaidi Tume ya Uchaguzi Zanzibar na kufikia kuwa Mwenyekiti wa
Tume ya Uchaguzi ya Nchi za Kusini na Mashariki mwa Bara la Afrika { Sadc
}.
“ Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar { ZEC } imefikia daraja ya kuwa sehemu ya Tume ya Uchaguzi ya Umoja wa
Afrika { AU }”. Alifafanua Mwenyekiti huto wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Nd.
Mwinchande.
Aliipongeza Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuijengea uwezo Tume hiyo uliosaidia kufanikisha
majukumu waliyopangiwa baada ya kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa
watendaji wa wizara tofauti za Serikalini.
Akitoa pongezi zake kwa
kazi kubwa iliyotekelezwa na Wajumbe wa Tume hiyo ya Uchaguzi ya Zanzibar { ZEC
} Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema
Zanzibar imefanya kura ya maoni iliyopelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 kuingia
katika historia mpya ya amani na utulivu.
Balozi Seif alifahamisha
kwamba Uongozi makini wa Tume hiyo kwa kiasi kikubwaumesaidia kusimamia
kupunguza joto la kisiasa ndani ya visiwa vya Zanzibar lililodumu kwa kipindi
kirefu.
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar aliwahakikishia wajumbe wa Tume hiyo inayomaliza muda wake kwamba
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itajitahidi kuona Tume mpya itakayochaguliwa
itapatiwa vitendea kazi pamoja na fedha kwa lengo la kufanikisha kazi za
zake.
“ Tutahakikisha
changamoto zilizojichomoza ndani ya kipindi cha utumishi wenu wa miaka mitano,
Serikali inazipatia ufumbuzi wa kudumu”. Alisisitiza Balozi
Seif
[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Post a Comment