Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Club 327 yazindua vyumba maalum kwa wafanyabiara

 

Uzinduzi wa club 327 wikiendi hii ulihudhuriwa na wafanyabiashara mbalimbali ambao walipata fursa ya kuona vyumba maalumu kwa ajili ya kufanyia mazungumzo ya kibiashara au kubadilishana mawazo vilivyotengenezwa na kinywaji cha Moet na Chandon.

Vyumba hivyo maalumu vitatu, cha Moet na Chandon, Belvedere na Hennessy vimeunganishwa na huduma ya DSTV, majokofu yenye vinywaji wakati wote, bafu ya ndani kwa ndani, pamoja na muziki.

‘Vyumba hivi ni maalumu kwa kuwakutanisha marafiki wanaofurahia jambo fulani au wateja wanaojadili biashara mbalimbali’ alisisitiza bwana Kadri.
Hivi karibuni pia vyumba hivyo vitaunganishwa na mfumo wa simu ambapo wateja wanaweza kupiga simu kuagiza vinywaji, au kumpigia DJ kuomba mziki wanaoupenda au kupiga simu nje ya nchi.

‘Sehemu hakika imeandaliwa maalumu ili kuwapa wateja wafanyabiashara kitu ambacho kimekuwa kikikosekana sehemu nyingi za burudani’ alisitiza bwana Kadri, mmilikiwa Bar hiyo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top