Jengo la Benki ya CRDB Burundi. (Picha
zote kwa hisani ya Dar es Salaam Yetu Blog na This Day Magazine).
Rais wa Burundi Piere Nkurunziza akiwasili katika sherehe
za ufunguzi rasmi wa Benki ya CRDB jijini Bujumbura, Burundi. Benki ya CRDB
imekuwa Benki ya kwanza ya kizalendo kufungua tawi lake nchini
Burundi.
Rais wa Burundi, Mheshimiwa Piere Nkurunziza akikata
utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Benki ya CRDB nchini Burundi Kushoto
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei.
Rais wa Burundi Mheshimiwa Piere Nkurunziza akisalimiana
na Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Benki ya CRDB Tully Esther Mwambapa
alipokuwa akiwasili katika sherehe hizo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei
akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Burundi Dk. James Nzagi (Kushoto) na
Katibu wa Benki hiyo Bwana John Rugambo (wa pili kushoto) na Meneja Mkuu wa
Benki ya CRDB Nchini Burundi Bw. Bruce Mwile.
Rais wa Burundi Mheshimiwa Piere Nkurunziza akiwa katika
picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Benki ya CRDB.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB nchini Burundi wakiwa katika
picha ya pamoja na wafanyakazi wenzano kutoka Dar es Salaam
Post a Comment