Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

DEREVA WA BASI LA MSANYA TRANS LILILOUA 11 IRINGA ASOMEWA MASHTAKA 40 AKIWA WODINI ,AKANA YOTE

 






Mtuhumiwa wa ajali ya basi la Msanya Trans lenye namba za usajili T 803 AJV Nisani Bw Rashid Selemani Msanya (35) lililosababisha vifo vya abiria 1 na kujeruhi wengine 28 akiwa wodini katika Hospitali ya mkoa wa Iringa baada ya kusomewa mashtaka yake 40 na mahakama akiwa kitandani

Wagonjwa na ndugu wa wagonjwa waliolazwa katika wodi hilo wakishuhudia tukio hilo baada ya hakimu mkazi ,mwandamizi mfawidhi wa mahakama ya mkoa wa Iringa Juma Hasan kumaliza kushughuli za kimahakama Hospitalini hapo


DEREVA wa basi la Msanya Trans ambalo lilitapa ajali mbaya jumamosi ya wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu 11 na kujeruhi wengine zaidi ya 20 katika eneo la Kichakani kwenye barabara kuu ya Iringa -Mbeya amesomewa mashitaka 40 akiwa wodi
ni katika Hospitali ya mkoa wa Iringa.

Wakisoma mashtaka hayo leo katika wodi namba 5 Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ,mbele ya hakimu mkazi ,mwandamizi mfawidhi wa mkoa wa Iringa Juma Hassan wakili wa serikali Adolph Maganda akisaidiwa na msaidizi wake Hamad Magenda alisema kuwa mtuhumiwa huyo katika kesi hiyo namba 90 ya mwaka 2012 ya usalama barabarani anatuhumiwa kutenda makosa hayo Desemba 8 mwaka huu .

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo Bw Rashid Selemani Msanya (35) ambae alikuwa ni dereva wa basi hilo la Msanya Trans lenye namba za usajili T 803 AJV Nissan ambalo lilikuwa likitokea Iringa mjini kwenda Usokami wilaya ya Mufindi alisababisha ajali na kupelekea vifo vya watu 11 waliokufa katika ajali hiyo.

Wakili Magande alisema kuwa mtuhumiwa huyo anatuhumiwa kwa makosa 40 ambapo jumla ya makosa 11 ni ya kusababisha vifo na makosa 28 ni ya kusababisha majeruhi na kosa moja kati ya 40 ni kusababisha ajali na kuharibu gari hilo.

Hata hivyo mtuhumiwa huyo amekana makosa yote na kuendelea kuwa chini ya ulinzi wa polisi wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali hiyo ya mkoa wa Iringa akitibiwa majeraha makubwa ya moto ambao unasadikika kutokana na maji ya rejeta ya basi hilo.

Hakimu wa mahakama hiyo mheshimiwa Hassan alimnyima dhamana mtuhumiwa huyo hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Desemba 20 mwaka huu na kuwa mtuhumiwa ataendelea kuwa chini ya ulinzi wa polisi katika Hospitali
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top