Waziri
wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka
(kushoto), akimkabidhi kombe, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi katika
Benki ya CRDB, Esther Kitoka, baada ya benki hiyo kushika nafasi ya pili, katika
hafla ya utopaji tuzo za
Mwajiri Bora Tanzania 2012 zilizofanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Habari
Mseto Blog)
Baadhi ya maofisa wa benki ya CRDB wakiwa na
tuzo tatu walizoshinda katika hafla ya utoaji wa tuzo za Mwajiri Bora.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi katika Benki ya CRDB, Esther Kitoka
Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi katika Benki ya CRDB, Esther Kitoka
DAR ES SALAAM,
Tanzania
BENKI ya CRDB imejishindia
tuzo tatu ikiwamo ya Fedha kwa kushika nafasi ya pili katika kinyang’anyiro cha
Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2012, zilizohusisha zaidi ya Kampuni 30,
ambayo ilipokelewa na Naibu Mkurugenzi
Mtendaji Huduma Shirikishi wa benki hiyo Esther Kitoka.
Hafla ya kukabidhi tuzo hizo
zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri nchini Tanzania (ATE) , ilifanyika kwenye
Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ambapo Rais Jakaya Kikwete alikuwa
mgeni rasmi.
Akiongea wakati wa kukabidhi
tuzo hizo, Rais Kikwete, aliwashukuru waajiri Wakitanzania, mashirika ya umma na
binafsi kwa kazi nzuri waliyoifanya katika kuisadia Serikali kutengeneza ajira
na maendeleo ya uchumi na pia alikiri uwepo wa tatizo la ajira hapa
nchini.
“Ninayo furaha kushiriki
nanyi jioni ya leo. Mmekuwa msaada mkubwa kwa taifa letu na ninapenda kuwaahidi
kuwa Serikali itawasaidia katika shughuli zenu,” alisema Rais Kikwete.
Aidha Rais Kikwete aliongeza
kuwa, juhudi za Serikali pekee haziwezi kuifanya nchi ya Tanzania kuwa yenye
kipato cha kati labda kama kutakuwa na juhudi kati ya Serikali na sekta binafsi
ambazo zitasaidia kupunguza idadi ya Watanzania wasio na ajira
nchini.
Rais Kikwete ametoa
changamoto kwa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na Serikali kufanya kazi kwa
pamoja katika masuala mawili muhimu ambayo ni maendeleo ya rasilimali watu hasa
katika uendelezaji wa ushirikiano wa maendeleo kati ya taasisi za vyuo vya juu
na viwanda.


Post a Comment