Rais wa serikali ya Mpito ya Mali Diouncounda Traore amemteua waziri mkuu mpya ikiwa ni saa chache baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu kujiuzulu baada ya kulazimishwa na majeshi.
Katika uteuzi uliotangazwa katika televisheni, Django Sissoko (pichani) ameteuliwa kuchukua nafasi ya Cheick Modibo Diarra ambaye amekuwa chini ya ulinzi tangu kujiuzulu kwake.
Kitendo cha jeshi kulazimisha kujiuzulu kwa Bw. Diarra kumeshutumiwa na Umoja wa mataifa na mataifa mengine kadhaa.
Hata hivyo Kapteni Amadou Sanogo aliyeongoza mapinduzi ya mwezi Machi amesema Bw. Diarra hakulazimishwa kujiuzulu na jeshi hilo.


Post a Comment