Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

FIFA CLUB WORLD CUP 2012: MONTERREY 1 vs CHELSEA 3

 


Chelsea wameanza Mashindano yao ya kwanza kabisa ya FIFA kusaka Klabu Bingwa Duniani kwa kuifunga Monterrey ya Mexico Bao 3-1 katika Nusu Fainali iliyochezwa huko Japan hivi leo.
Wachezaji wa Chelsea wakipongezana
Mata akishangilia mara ya kufunga goli dakika ya 17
Sasa Chelsea watacheza Fainali hapo Jumapili dhidi ya Klabu ya Brazil, Corinthians, ambao walifuzu Nusu Fainali yao hapo jana kwa kuwafunga Mabingwa wa Afrika, Al Ahly, Bao 1-0.
Al Ahly na Monterrye zitacheza hio Jumapili kabla ya Mechi ya Fainali kutafuta Mshindi wa Tatu wa Mashindano haya.
Chelsea walitangulia kupata Bao zao 3 kupitia Juan Mata, Fernando Torres na la tatu alifunga alijifunga mwenyewe Mchezaji wa Monterrey Darvin Chavez alipotumbukiza wavuni krosi ya Mata.
Katika Dakika za majeruhi, Monterrey walipata kifutia machozi kwa Bao la Aldo de Nigris.
Katika Mechi ya leo, kivutio kikubwa ni kumwona Sentahafu David Luiz akicheza vizuri kama Kiungo, akiziba vizuri pengo la Kiungo Oriol Romeu ambae aliumia Wiki iliyopita na inasemekana atakuwa nje ya Uwanja kwa Miezi 6.
Chelsea hapa walishangilia mpaka kocha wao Rafael akafurahiRafael Benitez akifurahia ushindi uwanjani hapo leo mchana Dadaz wa kijapan ambao pia ni mashabiki wa Chelsea wakitokelezea kwa ishara ya Peace & love hapa.
VIKOSI:
MONTERREY: OrOrozco, Perez (Osorio 58), Mier, Basanta, Chavez, Meza (Solis 83), Ayovi, Cardozo, Corona, Delgado (Carreno 83), De Nigris.
Goals: De Nigris 90+2.
CHELSEA: Cech, Azpilicueta, Cahill, Ivanovic, Cole, Mikel, Luiz (Lampard 63), Mata (Ferreira 74), Oscar, Hazard, Torres (Moses 79).
Goals: Mata 17, Torres 46, Chavez OG 48.
Attendance: 36,648
Referee: Carlos Vera (Ecuador)


MAGOLI:
Monterrey 1
-De Nigris Dakika ya 90
Chelsea 3
-Mata Dakika ya 17
-Torres 46
-Chavez 48′ (Kajifunga mwenyewe)



RATIBA:
MSHINDI wa 3
Desemba 16
[Uwanja wa Yokohama]
[Saa 4 na Nusu Asubuhi]
Al Ahly v Monterrey
FAINALI
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Corinthians v Chelsea



MABINGWA WALIOPITA:
-2000 - Corinthians
-2005 - Sao Paulo
-2006 - Internacional
-2007 - AC Milan
-2008 - Manchester United
-2009 - Barcelona
-2010 - Inter Milan
-2011 – Barcelona

KLABU BINGWA DUNIANI 2012
TIMU ZITAKAZOSHIRIKI:
Chelsea-BINGWA ULAYA
Corinthians-BINGWA MAREKANI ya KUSINI
Monterrey-BINGWA MAREKANI ya KATI NA KASKAZINI
Auckland City-BINGWA KANDA ya OCEANIA
Usain Hyundai-BINGWA-Barani Asia
Al Ahly-BINGWA-Barani Afrika
Sanfrecce Hiroshima-BINGWA-Japan J-LIGI

RATIBA/MATOKEO:
Raundi ya Mchujo - Desemba 6, Yokohama
Sanfrecce Hiroshima 1 Auckland City 0
ROBO FAINALI - Desembar 9, Toyota
Usain Hyundai 1 Monterrey 3
Sanfrecce Hiroshima 1 Al Ahly 2
MSHINDI wa 5- Desemba 12, Toyota
[Saa 4 na Nusu Asubuhi]
Usain Hyundai 2 Sanfrecce Hiroshima 3

NUSU FAINALI
Desemba 12, Toyota
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Al Ahly 0 Corinthians 1
Desemba 13, Yokohama
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Monterrey 1 Chelsea 3

MSHINDI wa 3
Desemba 16
[Uwanja wa Yokohama]
[Saa 4 na Nusu Asubuhi]
Al Ahly v Monterrey

FAINALI
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Corinthians v Chelsea
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top