CAF
KUFANYA UKAGUZI WA ‘LESENI ZA KLABU’ JANUARI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litatuma ofisa wake nchini mwezi ujao kwa ajili
ya kufanya ukaguzi kwenye klabu za Ligi Kuu ya Tanzania kabla ya kutoa leseni
kwa zile ambazo zitakuwa zimekidhi vigezo vilivyowekwa. Ili klabu ishiriki
mashindano ya CAF ni lazima iwe na leseni hiyo.
Kwa
mujibu wa CAF, ofisa huyo atakuwa nchini kuanzia Januari 7 mwakani ambapo
atafanya ukaguzi huo hadi Januari 14 mwakani. Mbali ya ukaguzi katika klabu, pia
ofisa huyo atakagua viwanja vitakavyotumika katika mashindano yake na hoteli
ambazo timu kutoka nje zitakuwa zinafikia kabla ya
mechi.
Baadhi
ya masharti kabla ya klabu kupewa leseni ya CAF ni pamoja na kuwa na ofisi
(physical address), uwanja wake wa mazoezi, programu ya maendeleo kwa vijana,
sekretarieti ya kuajiriwa, hesabu za fedha zilizokaguliwa (audited accounts) na
benchi la ufundi linaloundwa na watu wenye sifa zinazostahili.
PONGEZI
KWA UONGOZI MPYA DRFA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaupongeza uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika
juzi (Desemba 12 mwaka huu) hoteli ya Mbezi Garden.
Ushindi
aliopata Almasi Kasongo aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti pamoja na wajumbe wengine
wa Kamati ya Utendaji unaonesha jinsi ambavyo wajumbe wa Mkutano Mkuu wa DRFA
walivyo na imani kwao.
TFF
inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya DRFA ambayo hivi
sasa ina kinara mpya, na kwamba ina changamoto kubwa ya kuhakikisha inaendesha
shughuli za DRFA kwa kuzingatia katiba na kanuni.
Pia
tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA chini ya Juma Simba na Kamati ya
Uchaguzi ya TFF inayoongozwa na Deogratias Lyatto kwa kuhakikisha uchaguzi huo
unafanyika kwa utulivu na kwa kuzingatia katiba na Kanuni za Uchaguzi za
Wanachama wa TFF.
Safu
mpya ya uongozi wa DRFA inaundwa na Kasongo (Mwenyekiti), Meba Ramadhan (Makamu
Mwenyekiti), Msanifu Kondo (Katibu), Muhsin Said (Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa
TFF), Benny Kisaka (Mwakilishi wa Klabu), Ally Hobe (Mhazini) na wajumbe Mohamed
Shabani, Sunday Mwanahewa na Bakari Mapande



Post a Comment