Mtibwa
Sugar ya Morogoro leo asubuhi (Desemba 14 mwaka huu) imeibuka na ushindi wa
mabao 3-1 dhidi ya Toto Africans ya Mwanza katika mechi ya michuano ya Kombe la
Uhai inayoshirikisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U20) za klabu
za Ligi Kuu ya Vodacom.
Juma
Luzio alifunga mabao yote matatu (hat trick) katika mechi hiyo iliyochezwa
Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam. Alifunga mabao hayo dakika
za 44,81 na 88.
Hata hivyo, Toto Africans ndiyo
walioanza kufunga katika mechi hiyo ya kundi A. Bao hilo katika michuano hiyo
inayodhaminiwa na kampuni ya Said Salim Bakhresa kupitia maji Uhai lilifungwa
dakjika ya 22 na Pastol Makula.
Nayo
Simba imenguruma baada ya kuitandika Mgambo Shooting ya Tanga katika mechi
nyingine ya michuano hiyo iliyochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa Azam ulioko
Chamazi. Wafungaji kwa washindi walikuwa Ramadhan Mdoe dakika ya 19, Mohamed
Salum dakika ya 77 na Ramadhan Singano dakika ya
89.
Michuano
hiyo inaendelea leo mchana na jioni. Mechi ya Ruvu Shooting na Kagera Sugar
iliyokuwa ichezwe mchana Uwanja wa Azam, Chamazi sasa itafanyika saa 10 kamili
jioni katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Mechi
nyingine za leo ni Coastal Union vs JKT Ruvu (mchana- Karume), African Lyon vs
Azam (jioni- Chamazi). Vilevile mechi kati ya JKT Oljoro na Yanga inachezwa leo
Uwanja wa Chamazi.
Kesho
(Desemba 15 mwaka huu) ni mapumziko, na michuano hiyo itaendelea Jumapili kwenye
viwanja vyote viwili- Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na Uwanja wa Azam-
Chamazi.



Post a Comment