Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HABARI ZA KIMATAIFA ZILIZOTIKISA DUNIA

Rais wa Ghana afariki dunia.



Taarifa za habari kutoka Ghana zinasema rais John Atta Mills amefariki dunia. Ofisi ya rais inasema kiongozi huyo aliyekuwa na umri wa miaka 68 alifariki ghafla leo masaa machache baada ya kuugua.Taarifa za habari za Ghana zinasema alifariki katika hospitali ya jeshi kwenye mji mkuu Accra. Hakuna maelezo ya haraka juu ya kifo chake.John Atta Mills aliongoza Ghana tangu mwaka 2009.


Mohammed Morsi Rais Mpya wa Misri

Mohamed Morsi
alitangazwa mshindi hapo siku ya jumapili tarehe 24 juni katika uchaguzi wa Rais nchini Misri.Mursi ameshinda kwa asilimia 51.7% akimshinda mpinzani wake wa karibu Ahmed Shafik kwa mujibu wa tangazo la tume ya uchaguzi wa juu wa Rais.



Waziri Mkuu Wa Zamani Wa Italia, Berlusconi, Afungwa Miaka 4!

Ni kwa kosa la ukwepaji kodi.

MELES ZENAWI AFARIKI DUNIA

Marehemu Meles Zenawi, aliyekuwa waziri mkuu wa Ethiopia
Waziri mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi, amefariki dunia Jumatatu Agosti 21, 2012, wakati akipokea matibabu nchini Ubelgiji.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, Bereket Simon, alitangaza maombolezo ya kitaifa mjini Addis Ababa kufuatia kifo hicho.

Televisheni ya nchi hiyo ilisema, mwli wake utasafirishwa nyumbani Ethiopia kutoka ubelgiji, naibu waziri mkuu,Hailemariam Desalegn atachukua nafasi ya kiongozi huyo.

Kiongozi huyo mwenye amefariki akiwa na umri wa miaka 57, ni miongoni mwa viongozi wa Afrika waliokaa muda mrefu madarakani na habari zinasema, kwa wiki kadhaa alikuwa haonekani hadaharani.

Kwa mujibu wa televisheni hiyo ya serikali, Zenawi alifariki usiku wa jumatatu kuamkia Jumanne, ambapo alikuwa anapata nafuu kabla ya kuzidiwa tena ghafla.
Picha za hivi karibuni za televisheni, zilionyesha Zenawi akiwa amekonda.

Zenawi alianza kutawala kama rais wan chi hiyo manamo mwaka 1991, na baadaye kuwa waziri mkuu mwaka 1995
Kwa muda mrefu, Zenawi alichukuliwa na Marekani kama mshirika muhimu kiusalama, ambapo alikuwa akipokea mamilioni ya dola.

 

OBAMA ACHAGULIWA TENA KUINGOZA MAREKANI



Mitt Romney, baada ya kushindwa uchaguzi

 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top