
Mwamuzi Sylvester Kirwa kutoka Kenya ndiye atakayechezesha mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Taifa Stars na mabingwa wa Afrika, Zambia (Chipolopolo) itakayofanyika Desemba 22 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kirwa anayetambuliwa na Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) atasaidiwa na Elias Wamalwa na Marwa Range.
Waamuzi hao wasaidizi ambao vilevile watatoka Kenya
pia wanatambuliwa na FIFA.
Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager tayari iko kambini hoteli ya Tansoma, na inafanya
mazoezi katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na ule wa Uwanja wa Taifa kwa
ajili ya mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake


Post a Comment