WANAJESHI nchini Misri wameanza kuwaondoa watu kutoka katika eneo la Ikulu ya rais mjini Cairo ambako kumekuwa na makabiliano makali kati ya wafuasi na wapinzani wa rais Mohammed Morsi. Limetuma vifaru na magari mengine yaliyo hamiwa kwa silaha nje ya kasri la rais baada ya mapigano ya usiku kucha kati ya wafuasi na wapinzani wa Rais Mohammed Morsi.
Walioshuhudia matukio
wanasema kuwa waandamanaji wameanza kuondoka kutoka eneo hilo. Makabiliano
yamesababisha vifo vya watu watano na wengine zaidi ya mia sita wakijeruhiwa.
Taarifa za televisheini ya taifa zinasema kuwa rais Morsi atatoa hutuba kwa
taifa baadaye leo.
Mamlaka Kuu ya
Waisilamu, Al-Azhar, imemtaka rais kufutilia mbali mamlaka aliyojilimbikizia.
Viongozi wa upinzani wameitisha maandamano zaidi hii leo kupinga hatua ya rais
kujipa mamlaka zaidi pamoja na kuipinga rasimu ya katiba mpya inayotarajiwa
kupigiwa kura tarehe 15 mwezi huu.
Pande hizo mbili
zilitumia mawe, na mabomu ya petroli kushambuliana baada ya wafuasi wa rais
kujaribu kulitawanya kundi la upinzani lililokuwa likiandamana nje ya kasri la
rais. Upinzani umeshutumu chama cha Muslim Brotherhood kupanga mashambulio hilo
Vurugu hizo zilisambaa katika maeneo mengine ya nchi hiyo huku ofisi za Muslim
Brotherhood zikishambulia katika miji ya Ismailia na Suez.
Washauri wanne wa rais
Morsi wamejiuzulu. Upinzani unasema upo tayari kwa mazungumzo iwapo Morsi
atasitisha agizo linalompa mamlaka mpaya ya zaidi na iwapo ataahirisha kura ya
maoni ya kielelezo cha katiba.
Post a Comment