Mwenyekiti wa jUkwaa la Katiba Tanzania Bw. Deus Kibamba (kushoto) akizungumzia Uharakishaji wa Katiba Unavyoanza kuleta Fujo na kuathiri Ushiriki wa Wananchi katika Uundaji wa katiba Mpya ambapo pamoja na mambo mengine pia amezungumzia baadhi ya mapungufu kuwa ni Fursa finyu ya utoaji maoni, wakuu wa Wilaya na Mikoa kuzuia uhamasishaji, Vyama kuendelea kuingilia mchakato na makundi Maalum kuendelea kunyimwa haki ya kushiriki. Katikati ni Mratibu Jukwaa la Katiba Tanzania Bi. Diana Kidala.