MACHINGA wa Mji wa Moshi
leo walileta kizaa zaa katika mji wa Moshi baada ya Wafanya biashara hao wadogo
kufunga barabara ya Ghala, wakipinga kitendo cha Uongozi wa Manispaa ya Moshi,
kuvunja Gereji ya Bantu, wanayoitumia kama sehemu ya kuhifadhia bidhaa
zao.
Akizungumza na Machinga hao
katika juhudi ya kuhakikisha usalama unarejea kama kawaida, RCO Nga’azi
aliwataka viongozi wa Wamachinga kuwatuliza wafuasi wao, nakuangalia njia
nyingine ya kutafuta haki kwa amani.
Alisema kuna umuhimu wa
kila mwananchi kutambua wajibu wa kudumisha amani na kuwakumbusha umuhimu wa
kuhakikisha haki wanayoitafuta haikiuki haki za binadamu na Raia wengine wa nchi
hii.
Akizungumza na wamachinga
hao, muda mfupi baada ya kuwasili katika eneo la tukio, Mkuu wa wilaya ya Moshi,
Dkt. Ibrahimu Msengi, aliwaahidi wachinga hao kufanyia kazi tatizo lao na
kuwaomba wateue wawaklishi wao wanne ambao aliandamana nao hadi katika ofisi ya
mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Bernadeta Kinabo, kuzungumza Tatizo na
kulipatia ufumbuzi.
“Nimesikia tatizo lenu na
kilio chenu ndio maana niko hapa, nataka niwahakikishie kwamba le oleo mtapata
majibu kutoka kwangu, kwa sasa ninachowaomba nim kila mtu arejee katika shughuli
zake za kawaida ili amani ya mji wetu uendele kuwepo,” alisema
Msengi.
Kwa upande wao, baadhi ya
Machinga wanaodaiwa kuvunjiwa na kuharibiwa mali zao katika tukio hilo
lililotokea jana , majira ya saa saba usiku, Abdallah Abushehe na Mwamedi Ally,
walisema kuwa, asubuhi ya leo waliamka na kufika katika gereji hiyo wanayo
itumia kuhifadhia bidhaa zao na kukuta eneo hilo limevunjwa na baadhi ya mali
zao kupotea.
“Mimi ni fundi viatu,
kawaida yetu ni kuhifadhi bidhaa zetu hapa gereji, wamevunja usiku usiku hata
taarifa hawajatupa, hawa wagambo wamezidi kutuonea sana, kila siku wanatukimbiza
wanatunyima raha kweli ya kufanya kazi, sasa hivi mkokoteniwangu na magunia
yangu ya viatu siyaoni, kwa kweli sisi tumechoshwa na uongozi wa Manispaa,”
alisema Ally.
Naye mmiliki wa Gereji ya
Bantu lililovunjwa na kuzaa mzozo huo, Abdillahi Ally, alikiri kupata taarifa
kutoka kwa Mkurugenzi wa mji wa Moshi, Bernadetta Kinabo kuhusu eneo hilo kuwepo
katika ramani za ujenzi wa Nyumba za shirika a Nyumba Taifa
(NHC).
Alisema kuwa aliwahi kupata
Barua kutoka kwa Meneja wa NHC, iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi,
ikimtaka kuachia sehemu hiyo ndani ya siku mbili, lakini kutokana na kutoridhika
na maamuzi ya hayo alifungua kesi Mahakamani.
Post a Comment