DAR
ES SALAAM, Tanzania
KIONGOZI
wa Kanisa Katoliki Tanzania, Muashamu
Kadinali Polycarp Pengo (pichani juu), amewaonya
baadhi ya wanasiasa na taasisi kuacha
kuwashinikiza wananchi kutoa maoni ya mchakato Katiba Mpya kwa ajili ya maslahi
yao binafsi.
Kadinali Pengo aliyasema hayo
wakati alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,
kuhusu ujumbe uliotolewa na maaskofu kwenye mkutano wa viongozi hao,
uliyofanyika Oktoba 7 hadi 28 mwaka huu, huko Rome,
Italia.
Alisema kwa kuwa Katiba
linagusa maslahi ya nchi hivyo ni vyema kila mwananchi akatumia fursa yake ya
kuwasilisha maoni yake mwenyewe.
“Watu waruhusiwe kutoa maoni
yao, lakini lazima tukubaliane kuwa kila mtu ana maoni yake na maoni yote
hayewezi kuingizwa katika katiba hiyo,” alisema.
Alisema kuna mfumo ambao
baadhi ya nchi umetumia kwa kuandaa katiba mbili kisha kutafutwa watu maalumu
wakukabidhiwa katiba hizo kisha wakaandaa katiba mpya.
Katika hatua nyingine Kanisa
hilo limewataka viongozi wenye dhamana kuacha kushabikia udini katika kusimamia
haki za jamii ya Kitanzania.
Askofu Pengo alisema wapo
watu makini wenye uwezo wa kusimamia mchakato huo ikiwemo Tume iliyoteuliwa
kusimamia mchakato huo.
Alisema nchi hii imegawanyika
katika madhehebu mbalimbali hivyo, inapotokea dhehebu moja kulitukana na
kuharibu mali za lingine, serikali haipaswi kukaa kimya bali inachotakiwa ni
kusimamia haki za makundi yote na si kubagua.
“Suala Sheikh Ponda
sijalifuatilia lakini kama kweli hayo yaliyotokea kwa kuchomwa makanisa, lazima
serikali ishughulikie uharibifu wa mali hizo za dini na madhehebu yote haipaswi
kubagua”alisema
Askofu Pengo alisema endapo
serikali itaamua kulishughulikia suala hilo kwa upande mmoja na kuacha maswali
kwa wengine basi itakuwa imekwenda kombo.
Alibainisha kuwa malalamiko
yanapotolewa na mtu kama yeye huwa hayana nguvu sana katika jamii kuliko
yanapotolewa na Rais wan chi.
Askofu Pengo alisema Rais ana
ngucu kubwa kwamba kila analolisema huwa linapokelewa kwa uangalifu mkubwa
katika.
“Ni lazima viongozi
wajiepushe katika kupenda ubaguzi wa kdini kwa mfano Mkapa hakuweza kusema
wakatoliki wenzangu na nyiye wenye mapenzi mema kwa lengo la kutekeleza majukumu
ya maendeleo”alisema.
Askofu Pengo alitoa tahadhari
kuwa Rais siyo lazima awe Mkatoliki au muislam, bali anapochaguliwa anakuwa Rais
wa nchi hii ilikuwatumikia watu wote ambapo pia anapaswa kulinda, kusimamia na
kulinda mali za madhehebu yote na si vinginevyo.
Akizungumzia kuhusu ujumbe wa
heri ya Chrismas na mwaka mpya, ambao ni kutoka kwenye mkutano huo, wa Rome na
kuelekezwa katika Bara la Afrika, Askofu Pengo alisema maskofu wa Sinod,
wamewapongeza waumini wao kwa kudumisha imani.
Alitanabaisha kuwa licha ya
mazingira magumu ikiwemo uchumi duni, njaa maradhi na imani potofu za kidini,
bado wameweza kustahimili na kuwafanya kubaki kitu kimoja.
Vilevile alisema Kanisa
limeweza kuwaleta kaleta waamini karibu na kuwa familia ya mungu ambapo kwa
Afrika neno familia lina maana kubwa kwani hujenga udugu na ujamaa katika
jamii.
Askofu Pengo alibainisha kuwa
familia ya mungu haibaki katika dhehebu fulani, bali neno hilo linasaidia kuwa
watu wote wenye mapenzi mema kuwa wa familia moja.
“Kutofautiana katika jamii ni
jambo la kawaida na kisha watu hurudi na kubaki familia moja”alisema
Aidha, kuhusu mihadhara ya
kidini, Askofu Pengo alisema hakuna mtu mwenye haki ya kumtukana mtu kutokana na
imani yake.
Alisema kama serikali
inashindwa kuwakemea wanaowatukana wengine anaogopa, hali ikiachwa iendelee
hivyo ianaweza kuvuruga amani na mshikamano na nchi kuingia kwenye
mgogoro.
Alisema haoni tatizo kama mtu
atasema Yesu si mwana wa Mungu katika nia ya mtazamo wake hapo kutakuwa hakuna
tatizo kwa kuwa hata yeye anaweza kusema Mohamed siyo Mtume tena kwa ushahidi
kutokana wa vitabu vya dini alivyosoma.
Kuhusu elimu nchini, Askofu
Pengo alisema watu wote wenye nia njema na mapenzi ya nchi hii wanapaswa kutoa
kipaumbele ili kila Mtanzania apate elimu iliyo bora.
Alisema hapendezwi na mpango
wa elimu inayotolewa nchini kwani mfumo wa baadhi ya shule nyingi zimekuwa
kitega uchumi hivyo kuwa kikwazo kwa watu wenyekipato cha
chini.
Askofu Pengo alisema hali
hiyo ikiachiwa iendelee inaweza kuja kuwafanya wale waliokosa elimu kuvuruga
amani kwa kudaai haki zao za kioungozi na maslahi mengine.


Post a Comment