Mwanamuziki kutoka nchini
DRC-Congo,Koffi Olomide akitia saini moja ya bango lenye kampeni
inayowatahadharisha madereva wa magari kunywa pombe kupindukia,ikiwa ni hatari
kwa afya na usalama wao kwa ujumla,pichani kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya bia
ya Serengeti,Bwa.Steve Gannon akishuhudia tukio hilo,aidha katika tukio hilo
Wanahabari mbalimbali walishuhudia tukio hilo ndani ya hotel ya Serena Inn
mapema leo mchana.Koffi Olomide na skwadi lake la Quartie Latin wametua jana
jijini Dar kwa ajili ya maonesho yao mawili yatakayofanyika jijini Dar ndani ya
viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni siku ya jumamosi na jijini Mwanza kwenye uwanja
wa CCM-Kirumba siku ya jumapili kwa udhamini mkubwa wa kampuni ya SBL kupitia
bia yake ya Tusker Lager.
Bango alilotia wino Koffi
Olomide.

Koffi Olomide akitoa
vionjo vya moja ya wimbo wake mbele ya wanahabari,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mahusiano Serengeti Breweries,Nandi
Mwiyombela akinogesha

Mkurugenzi wa Masoko
kampuni ya SBL,Ephraim Mafuru akiuzumguza mbele ya Wanahabari mapema leo ndani
ya hotel ya Serena Inn,kuhusiana na onesho la Mwanamuziki kutoka DRC-Congo,Koffi
Olomide linalotarajiwa kufanyika kesho jumamosi kwenye viwanja vya Lidaz
Club,Kinondoni jijini Dar.

Baadhi ya wafanyakazi wa
SBL wakifurahia jambo

Mkurugenzi wa Mahusiano Serengeti Breweries,Nandi
Mwiyombela akiwakaribisha wageni mbalimbali wakiwemo wanahabari kwenye mkutano
uliohusu onesho la Mwanamuziki Koffi Olomide,ambalo limedhaminiwa na kampuni ya
SBL kupitia kinywaji chake cha Tusker.

Mwanamuziki kutoka nchini DRC-Congo,Koffi Olomide
akifafanua jambo mapema leo alipokuwa akizungumza na wanahabari (hawapo
pichani),ndani ya hotel ya Serena kuhusiana na onesho lake atakalolifanya hapo
kesho ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Koffi amewaomba washabiki na wapenzi wake
waje wajionee kazi kubwa atakayokuwa akiifanya jukwaani akiwa na vipaji vipya
kabisa katika tasnia ya muziki wa dansi nchini Congo.

Mkurugenzi wa kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Steve
Gannon akimkaribisha Koffi Olomide (hayupo pichani) na pia aliwataka mashabiki
na wapenzi wa mwanamuziki huyo wajitokeze kwa wingi na kushuhudia tukio hilo
adhimu hapo kesho.

Mkurugenzi wa Clouds Media
Group,Joseph Kusaga akiwashukuru Wadhamini wa onesho la Koffi Olomide pamoja na
Wanahabari kwa ushirikiano mkubwa walioutoa katika kuhakikisha jamii inapata
taarifa mbalimbali kuhusiana na ujio wa mwanamuziki huyo pamoja na onesho
lenyewe.

Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya SBL,Ephraim Mafuru
akisalimiana mkono na Mwanamuziki wa Kimataifa Koffi Olomide.

Mkurugenzi wa Clouds Media
Group,Joseph Kusaga pichani shoto akiwa ameambata na mgeni wake Koffi Olomide
sambamba na Mkurugenzi wa SBL,Steve Gannon wakiwasili ndani ya ukumbi wa
mikutano,Serena Hotel kwa ajili ya kuzungumza na Wanahabari kuhusiana na onesho
litakalofanyika kesho kwenye viwannja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini
Dar.




Post a Comment