Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai akitoa taarifa yake ya uchaguzi wa kamati ya siasa ya mkoa kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha).(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu
Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida kimechagua kamati yake ya siasa mkoa katika uchagzui uliofanyika wiki iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai, amewataja wajumbe wa kamati hiyo, kuwa ni pamoja na mbunge wa viti maalum mh. Martha Mlata.
Amewataja wengine kuwa ni mbunge wa jimbo la Manyoni Magharibi, John Paulo Lwanji, Huseein Nagi na Mohammed Ghamayu.
Amesema wajumbe wengine ni MNEC ni mbunge wa jimbo la Singida kaskazini mh. Lazaro Nyalandu na MNEC wa wilaya ya Ikungi Jonathan Njau.
Amesema katika taarifa hiyo, wameagiza viongozi na wataalam wa kilimo kuhakikisha pembejeo zinawafikia wakulima kwa wakati.
Wakati huo huo, Msindai amesema mkutano huo umeagiza CCM katika ngazi zote, kubuni na kuanzisha miradi ya kiuchumi itakayosaidia kuondokana na utegemezi kutoka CCM makao makuu.
Post a Comment