KUMETOKEA
ghasia kadha kaskazini mwa Nigeria katika
eneo la mbali kaskazini-mashariki mwa nchi, watu wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa
kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Boko
Haram,
walishambulia kanisa, kituo cha
polisi, na ofisi za uhamiaji na ushuru katika mji wa Gamboru-Ngala, karibu na
mpaka wa Cameroon.
Askari
polisi wawili waliuwawa.
Pia
kumetokea mapambano baina ya watu waliokuwa na silaha na askari wa usalama
kwenye mji wa Azare, katika jimbo la Bauchi, kaskazini mashariki mwa
nchi.
Wakaazi wa
huko wanasema washambuliaji wawili waliuwawa na wa tatu amejificha ndani ya
nyumba ambayo sasa imezingirwa na polisi.


Post a Comment