Wananchi
wa Syria wakiangalia magari yaliolipuliwa na
mabomu.
MILIPUKO ya mabomu iliyotokea
kwa wakati mmoja katika kitongoji cha mji mkuu wa Syria Damascus imeuwa watu
wapatao 34.
Televisheni ya taifa ya Syria ilionyesha picha
za eneo la tukio eneo lenye wakristo wengi na waumini wa dhehebu la Druze .
Magari yaliyogonganishwa na milipuko hiyo na mabaki ya majengo yalichafua
mitaa.
Wanaharakati wanasema kuna ishara kwamba
kulikuwa na milipuko mingine midogo miwili zaidi ingawa haikuwa wazi kama mtu
yeyote alijeruhiwa.
Shirika la habari la SANA linasema shambulizi
hilo la leo ni kazi ya ugaidi , neno ambalo serikali ya Syria inatumia dhidi ya
majeshi ya wapinzani na waasi. Hii ni mara ya pili eneo hili limelengwa katika
miezi kadhaa iliyopita.
Post a Comment