Mmoja wa wawezeshaji
katika semina hiyo Bw. Thomas Bwana - Afisa Kilimo Mwandamizi kutoka Ofisi ya
Makamu wa Rais akiwasilisha mada juu ya Bioteknolojia ya
kisasa.
Mmoja wa wawezeshaji
katika semina hiyo Bw. Onesphory Kamukuru - Mhandisi wa Mazingira kutoka Ofisi
ya Makamu wa Rais akiwasilisha mada juu ya usimamizi wa matumizi salama ya
Bioteknolojia ya kisasa.
Katibu Mkuu Ofisi ya
Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula (kulia) akifungua rasmi semina ya watumishi wa
Ofisi yake kuhusu matumizi salama ya Bioteknolojia ya kisasa. Kushoto ni Naibu
Katibu Mkuu Eng. Ngosi Mwihava.
Baadhi ya Wafanyakazi wa
Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Katibu Mkuu Bw. Sazi Salula (hayupo
pichani) katika semina ya wafanyakazi wa Ofisi hiyo juu ya matumizi salama ya
Bioteknojia ya kisasa. Semina hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Karimjee
jijiini Dar es Salaam na kuwashirikisha wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais
kutoka Dar es Salaam, Zanzibar na Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya
Makamu wa Rais Sazi Salula akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi
yake kutoka Ofisi za Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar mara baada ya kufungua
semina ya matumizi salama ya Bioteknolojia ya kisasa.Picha na Ali
Meja
Post a Comment