Mikel Arteta, aliifungia
Arsenal bao la pekee na la ushindi wakati wa mechi yao ya leo dhidi ya
Wigan.
Ushindi huo ni wa tatu
mfululizo kwa Arsenal tangu mwezi mwaka huu.
Arouna Kone alipoteza
nafasi nzuri ya kuifungia Wigan wakati wa mechi hiyo wakati alipokuwa ndani ya
mstatili ya kupiga mkwaju ambao ulipaa juu ya mlingoti.
Arteta alifunga bao hilo
kupitia mkwaju wa penlti baada ya Jean Beausejour kumfanyia madhambi Theo
Walcott.
Wigan sasa imepoteza
mechi yake sita kati ya nane za ligi kuu na imesalia mkiani kwenye msururu wa
ligi kuu ya Premier kwa mwaka wa tatu mfululizo.
Katika mechi nyingine
Gareth Barry alifunga bao kunako dakika ya 92 na kusaida Manchester City
kuandikisha ushindi finyu didi ya Reading.
Matokeo zaidi
Kufuatia ushundi huo
Manchester City imasalia katika nafasi ya pili alama tatu nyumba ya Manchester
United ambayo inachuana na Swansea hiyo kesho.
Newcastle nayo
ilijizolea alama tatu muhimu pale ilipoilza Queens Park Rangers kwa bao moja kwa
bila.
Shola Ameobi ndiye
aliyeifungia Newcastle bao lake ya ushindi ambao pia ni bao lake la kwanza msimu
huu.
Steven Fletcher alifunga
bao lake na nane msimu huu na kuisadia timu ya Sunderland kuilaza Southampton
kwa bao moja kwa bila.
Ushindi huo sasa
umeinusuru Sunderland kutokana na tishio la kuwa miongoni mwa timu ambazo huenda
zikashushwa daraja.
Tottenham imetoka sare
ya kutofungana bao lolote la Stoke City kati mechi ya kusisimua iliyochezwa
katika uwanja wa White Hart Lane.
Kufuatia sare hiyo
Stoke, sasa imecheza mechi nane bila kupoteza na nusuru ifunga bao kunako dakika
ya kwanza, lakini mkwaju wa Kenwyne Jones ulipaa juu ya
mlingoti.
West Brom nayo
imesitisha rekodi ya Norwich ya kutoshindwa pale ilipoilaza kwa magoli mawili
kwa moja.
Everton ikatoka nyuma ya kufungwa bao moja na kushinda kwa magoli mawili kw moja dhidi ya West Ham United.
Everton ikatoka nyuma ya kufungwa bao moja na kushinda kwa magoli mawili kw moja dhidi ya West Ham United.
on Sunday, December 23, 2012
Post a Comment