Timu ya Taifa (Taifa Stars)
imeingia kambini jana jioni (Desemba 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam
kujiandaa kwa mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia
(Chipolopolo) huku Kocha Kim Poulsen akimjumuisha tena katika kikosi hicho kipa
Deogratias Munishi ‘Dida’.
Kocha Poulsen amemjumuisha
tena Munishi kwenye kikosi hicho kuziba nafasi ya Mwadini Ally ambaye atakuwa
nje ya nchi na timu yake ya Azam inayokwenda kushiriki mashindano maalumu nchini
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Wachezaji wote wengine
walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wamesharipoti
kambini hoteli ya Tansoma, na timu imeanza mazoezi leo asubuhi (Desemba 13 mwaka
huu) Uwanja wa Karume, na jioni itafanya mazoezi kwenye uwanja huo
huo.
Kuanzia kesho jioni (Desemba
14 mwaka huu) itafanya mazoezi Uwanja wa Uwanja wa Taifa wakati mazoezi ya
asubuhi yataendelea kuwa Uwanja wa Karume. Wachezaji ambao bado hawajaripoti
kambini ni Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaocheza mpira wa kulipwa nchini
DRC.
Mechi kati ya Taifa Stars na
mabingwa hao wa Afrika itachezwa Desemba 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa.
Kocha wa Chipolopolo, Herve Renard ameshataja kikosi chake cha wachezaji 24 kwa
ajili ya mechi hiyo.
COASTAL YAENDELEA KUCHACHAFYA
UHAI CUP 2012
Coastal Union ya Tanga
imeendelea kufanya vizuri kwenye michuano ya kuwania Kombe la Uhai
inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu ya
Vodacom baada ya jana (Desemba 12 mwaka huu) kuifunga Toto Africans mabao
3-1.
Mabao ya Coastal katika mechi
hiyo ya kundi A iliyochezwa Uwanja wa Chamazi yalifungwa na Mohamed Miraji
dakika ya 44, Abdul Banda (dk. ya 62) na Ramadhan Shame (dk. ya 83). Toto
Africans ndiyo iliyoanza kupata bao dakika ya 30 lililofungwa na Severin
Constantine.
Coastal Union ilishinda mechi
yake ya kwanza mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika michuano hiyo
inayodhaminiwa na kampuni ya Said Salim Bakhresa kupitia maji
Uhai.
Nayo Simba iliibuka na ushindi
wa mabao 2-1 dhidi ya African Lyon katika mechi ya kundi B iliyochezwa leo
asubuhi (Desemba 12 mwaka huu) Uwanja wa Karume. Miraji Athuman na Ramadhan Mzee
ndiyo walioifungia Simba dakika ya 15 na 47 wakati la African Lyon lilifungwa
dakika ya 57 na Mbela Kashakala.
Polisi Morogoro iliifunga Azam
bao 1-0 kwenye Uwanja wa Karume wakati katika Uwanja wa Azam, JKT Ruvu iliifunga
Tanzania Prisons bao 1-0 lililofungwa dakika ya 16 na Jacob Mambia. Yanga na
Ruvu Shooting zilitoka suluhu kwenye Uwanja wa Chamazi.
Katika mechi iliyochezwa leo
asubuhi (Desemba 13 mwaka huu) Uwanja wa Karume, Oljoro JKT imeizamisha Kagera
Sugar mabao 3-0. Mabao hayo yamefungwa na Hamis Saleh dakika ya 49 huku Shamir
Mohamed akipachika mawili dakika ya 52 na 55.
Michuano hiyo itaendelea kesho
(Desemba 14 mwaka huu) kwa michezo kati ya Mtibwa Sugar vs Toto Africans
(asubuhi- Karume), Coastal Union vs JKT Ruvu (mchana- Karume), Oljoro JKT vs
Yanga (asubuhi- Chamazi), Ruvu Shooting vs Kagera Sugar (mchana- Chamazi),


Post a Comment