Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Kocha mpya wa Simba Patrick Liewing atua jijini Dar

 

 

Kocha mpya wa Simba, Mfaransa, Patrick Liewing


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kocha mpya wa Simba, Mfaransa, Patrick Liewing pichani, aliyeshika nguo nyekundu mkononi, amewasili leo saa saba za mchana kwa ajili ya kuinoa timu ya Simba.

 Uongozi wa Simba, kwa kupitia Katibu Mkuu wao, Evodius Mutawala, alikuwa miongoni mwa wadau wa michezo waliompokea Liewing katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

Kocha huyo anawasili huku akiikuta timu ya Simba ikiwa chini ya Jamhuri Kihwelo Julio, kocha ambaye amekuwa na mapenzi makubwa na klabu hiyo kila wakati kwa kitendo chake cha kukubali kuinoa timu hiyo.



Mengi juu ya ujio wa kocha huyo raia wa Ufaransa, yatasikika baada ya kufanya mazungumzo ya mwisho na kuingia makubaliano rasmi ya kuinoa Simba, yenye kipindi kikubwa cha kurudisha imani kwa wapenzi na wanachama wao.

Simba ilimaliza mzunguuko wa kwanza wa ligi ya Tanzania kwa kushika nafasi ya tatu, nyuma ya timu ya Yanga na Azam FC.Habari picha kwa hisani ya http://handenikwetu.blogspot.com
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top