Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amelazwa hospitali kutokana na kuganda kwa damu baada ya kuumia kichwani hivi karibuni.
Wizara ya mambo ya nje inasema madaktari wa Clinton waligundua hali hiyo jana jumapili alipokwenda kwenye uchunguzi wa kawaida. Wamesema ilikuwa inahusiana na kujigonga kichwani baada ya kuanguka wiki kadhaa zilizopita.
Clinton anatibiwa na dawa za kusaidia damu kutokuganda katika hospitali ya Presbyterian huko New York. Anategemewa kubaki hospitali kwa uangalizi zaidi kwa siku mbili zijazo.
Taarifa imesema madaktari wa Clinton wataendelea kumwangalia na kuangalia kama kuna haja ya kuchukua hatua zaidi.
Post a Comment