Bango linaloonyesha
Idadi ya watu wote Watanzania, baada ya kuhesabiwa katika zoezi la kuhesabu
Sensa lililoanza mwezi Agosti mwaka huu na kufikia tamati hii leo wakati Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, alipotangaza rasmi matokeo
ya Senza ya watu na makazi na kutaja idadi kamili, wakati wa hafla hiyo
iliyofanyika leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam.
Rais Jakaya Kikwete,
akizungumza na wananchi wakati akisoma hotuba yake ya kutangaza rasmi uzinduzi
wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi, leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es Salaam. Rais Jakaya, alisema kuwa katika Sensa ya mwaka huu, watanzania
wameongezeka kwa asilimia kubwa ukilinganisha na Sensa iliyofanyika kwa mara ya
kwanza nchini ya mwaka 1967, ambapo Watanzania wote walikuwa ni Milioni 12, 313,
054, na Tanzania Bara walikuwa ni milioni 11, 958,654 na Visiwani Zanzibar,
walikuwa ni 354, 400, ambapo baada ya mwaka huo, Sensa kama hiyo ilifanyika tena
mwaka 1978, 1988,2002 na hii ya mwaka huu 2012, ambapo imetoa idadi ya
Watanzania wote kuwa ni jumla ya Milioni 44, 929,002.
Baadhi ya Madiwani na
viongozi mbalimbali wa Serikali, waliohudhuria katika hafla hiyo
leo.
Kikundi cha
Uhamasishaji cha Temeke, akikiwa ni miongoni mwa wageni waalikwa kilichokuwa
kikiendelea na kazi yake ya uhamasishaji uwanjani hapo.
Sehemu ya wananchi
waliojitokeza kuhudhuria hafla hiyo.
Bendi ya THT, kutoka
(kulia) ni Marlow, Amin na Linah, wakitoa burudani jukwaani wakati wa hafla
hiyo.
Wananchi wakisebeneka
kushangilia baada ya Rais Jakaya Kikwete, kutangaza rasmi matokeo hayo ya
Sensa.
Picha ya pamoja kwa
kumbukumbu.
Picha ya pamoja kwa
kumbukumbu.
Picha ya pamoja kwa
kumbukumbu.
Rais Jakaya Kikwete,
akiteta jambo na Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba, wakati akiondoka katika
viwanja vya Mnazi Mmoja, baada ya kuzidua rasmi matokeo ya Sensa ya watu na
makazi.
Post a Comment