CHAMA cha Soka mkoa wa
Kagera (KRFA), kimempinga Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar
Tenga na kamati yake ya utendaji kwa kupinga mchakato wa marekebisho ya Katiba
ya shirikisho hilo.
Mwenyekiti wa KRFA, Jamali
Malinzi amesema kuwa katika kikao cha kamati yake ya utendaji kilichoketi
Desemba Mosi mjini Bukoba wamekubaliana kutoshiriki mchakato wa marekebisho hayo
ya katiba yanayoendeshwa kwa njia ya waraka na kudai kuwa ni
batili.
"Mchakato wa TFF wa
kubadili katiba ya TFF kama ulivyoanishwa katika warakata wa TFF kwa vyama
wanachama wake ni batili kwa kuwa haukidhi matakwa ya katiba ya TFF kifungu cha
22 (1). Kifungu hicho cha 22 kinasema kuwa mkutano mkuu wa TFF ndio pekee wenye
mamlaka ya kubadili katiba ya TFF, aidha kifungu kidogo cha 30 1-6 kinaeleza
taratibu nzima ya mchakato wa kubadili katiba ikiwa ni pamoja na kutoa notisi ya
siku 45, kuitisha mkutano mkuu na kupigak ura na wajumbe theluthi mbili
kuridhia.
"Hakuna mahali popote
kwenye katiba ya TFF panapotamka kuwa katiba ya TFF itabadilishwa kwa wanachama
kuzungushiwa waraka kupiga kura na kuandika jina na saini na kisha kuituma kura
makao makuu ya TFF sisi kama KRFA hatutashiriki.
"alisisitiza Malinzi Mapema
wiki hii Rais wa TFF, Leodegar Tenga alisikika akisistiza kuwa mchakato huo wa
kubadili Katiba ya TFF kwa njia ya waraka uendelee kufanyika kwasababu
shirikisho hilo hivi sasa halina pesa za kuitisha mkutano mkuu kwa ajili ya
zoezi hilo na kuwataka wanachama wake kukubaliana na njia hiyo.
"Tunataka katiba yetu
ilindwe na iheshimiwe na watu wote mana katiba ndio muongozo mkuu wa vipi mpira
uendeshwe nchini mwetu, Katiba ya TFF ndio iliyomuweka Tenga madarakani pamoja
na kamati yake ya utendaji, katiba inatutawala wote hakuna aliye juu ya
katiba.
" alisema Malinzi
alionyesha kushangazwa na kauli ya TFF kudai kuwa ufinyu wa bajeti kuwa ni
kikwanzo kikuu kinachozuia mkutano mkuu wa kubadili katiba usifanyike. "TFF bila
kujali kama vyama vya mikoa vina pesa au la ilitoa ratiba ya chaguzi za mikoa na
kusisitiza ifuatwe, TFF haikutoa hata shilingi moja kusaidia zoezi hili, iweje
wao washindwe kama mikoa inayojiendesha bila vyanzo vyovyote vya mapato iliweza
sababu hii haina matinki.
"alisema kwa kuhoji Alisema
TFF inatakiwa kuitisha mkutano mkuu kwa mujibu wa katiba ya shirikisho hilo kwa
faida ya soka la Tanzania ikiwa ni pamoja na kuepukana na marumbano mbalimbli
yanayoweza kujitokeza endapo litakiuka taratibu.
Katika hatua nyingine,
Malinzi alisema kitendo cha kuwambia kipengele cha club licencing kisipoingizwa
kwenye katiba ya TFF basi vilabu vya Simba na Azam vitazuiwa kushiriki michuano
ya CAF mwakani ni kichekesho kwa kuwa TFF taarifa ya kutakiwa kuingizwa
kipengele hicho walikuwa nazo mapema toka mwaka 2006 kwenye mkutano wa Fifa
uliofanyika Berlin, Ujerumani mwaka huo na kusainiwa na Rais wa Fifa Sepp
Blatter Oktoba 29 mwaka 2007 na agizo hilo lilisisitizwa iwapo kipengele hicho
hakitaingizwa klabu hazitaruhusiwa kushiriki michuano ya CAF na
Fifa.
"Tenga ni mjumbe wa kamati
ya utendaji ya CAF baada ya kupokea waraka wa FIFA kuhusu suala hili alikaa na
kutoa ratiba ya mchakato wa utekelezaji wa agizo hilo, ratiba ilionyesha hadi
Desemba 2011 kila nchi mwanachama wa CAF ilitakiwa iwe imeingiza, siku saba
zimesalia tangu amalize muda wake wa uongozi Desemba 14 tunambiwa Simba na Azam
tusipotisha kipengele hiki hazitashiriki.
"Mwezi April mwaka huu TFF
ilifanya mkutano wake mbona hawakukiweka kipengele hiki kama ajenda?"alihoji na
kusema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 4.5.1. kwenye waraka wa FIFA kinaruhusu
nchi wanachama kuombea kibali klabu zake na kuitaka TFF kufanya hivyo kwa
kuziombea kibali cha kushiriki michuano ya CAF mwakani timu za Simba na
Azam.
Post a Comment