Mtu aliyejitambulisha
kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ),kambi ya Monduli,Arusha
akiwa na wabunge wa Chadema,Godbless Lema (Arusha Mjini) na Joshua Nassari
(Arumeru Mashariki) baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na
wabunge hao katika Mji mdogo Mererani,Simanjiro mkoani
Manyara.
MBUNGE wa
Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amesema kama angekuwa ndiye mwenye uamuzi
ya mwisho ndani ya Chadema, angempokea kwenye chama hicho askari wa Jeshi la
Wananchi Tanzania (JWTZ), aliyepiga naye picha kama kitendo hicho kitamfanya
afukuzwe kazi.
“Ingawa
wanaofaa kutoa kauli kama hizi ni viongozi wakuu kama Mwenyekiti na Katibu wa
Taifa kupitia vikao halali vya chama, lakini binafsi, ningekuwa na uwezo,
ningempokea mara moja askari huyu kwenye chama kama ishara ya walio tayari
kujitoa mhanga kupoteza vyote ikiwemo kazi kwa ajili ya ukombozi wa taifa iwapo
atafukuzwa kazi,” alisema Lema.
Hata hivyo,
Lema aliyekuwa akizungumza katika mahojiano maalumu akiwa mjini Moshi kwa
mapumziko ya Sikukuu ya Krismasi, alisema kitendo cha JWTZ kuanza kumwandama na
pengine kumfukuza kazi askari huyo, kitafumua chuki kubwa kati ya askari wa vyeo
vya chini na wenye vyeo vya juu ambao wengi wanaitumikia CCM kwa nafasi zao,
ukiwemo ukuu wa mikoa na wilaya.
Alitoa mfano
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Samuel Ndomba ambaye kabla ya kuhamishiwa Makao Makuu ya
jeshi alikoshika nyadhifa mbalimbali na hatimaye kuteuliwa kushika nafasi yake
ya sasa, alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, cheo kilichompa fursa ya kuwa mjumbe wa
Halmashauri Kuu na Kamati ya siasa mkoa wa CCM, Mkoa wa
Arusha.
“Askari huyu
mdogo akifukuzwa kazi kwa sababu ya picha aliyopiga na sisi, basi itathibitisha
double standard (undumila kuwili) ya utawala katika taifa letu. Huyu kapiga
picha na taarifa ya kusakwa inatolewa na JWTZ , lakini wako wengi ambao ni
wanajeshi wa vyeo vya juu ambao siyo tu wanapiga picha na viongozi wa chama
tawala bali ni wafanyakazi wa CCM kwa nyadhifa zao wakiwa bado wako jeshini,”
alisema Lema.
Alisema
ujasiri wa mtu huyo anayeamini kuwa kweli ni askari wa JWTZ kujitokeza kupiga
naye picha huku akijua anahatarisha kazi yake, ni ushahidi kuwa wapo askari
wengi nchini waliochoshwa na mwenendo wa CCM.
Alisema
ukweli huo unathibitishwa na matokeo ya kura katika vituo vilivyokuwa ndani au
jirani na vituo vya polisi na kambi za jeshi wakati wa uchaguzi mkuu uliopita,
ambapo wagombea wa upinzani walipata kura nyingi ikilinganishwa na wale wa
CCM.
Lema
aliyepiga picha na askari huyo akiwa na mbunge mwenzake wa Arumeru Mashariki,
Joshua Nassari (Chadema), alitoa changamoto kwa watu wenye mapenzi mema na taifa
hili, kufanya utafiti wa maofisa wa juu wa JWTZ na vyombo vingine vya ulinzi na
usalama wanaotumikia chama tawala kwa siri au kwa uwazi kupitia vyeo na nyadhifa
zao.
“Hawa ni pamoja na wakuu wa mikoa, wilaya na maofisa wa ngazi mbalimbali ndani ya CCM ambao tunashuhudia wakirejea jeshini wakitokea kwenye utumishi wa chama lakini hatujawahi kusikia tamko la kutafutwa wala kuchunguzwa na jeshi kwa kushiriki siasa,” alisema Lema.
“Hawa ni pamoja na wakuu wa mikoa, wilaya na maofisa wa ngazi mbalimbali ndani ya CCM ambao tunashuhudia wakirejea jeshini wakitokea kwenye utumishi wa chama lakini hatujawahi kusikia tamko la kutafutwa wala kuchunguzwa na jeshi kwa kushiriki siasa,” alisema Lema.
Alisema hata
ikitokea kweli askari aliyepiga naye picha akafukuzwa kazi hatajuta
kumsababishia madhila hayo bali atajisikia faraja kwa sababu kitendo hicho
kitafungua ukurasa mpyae katika harakati za ukombozi kwa watu kuelewa kuwa siyo
kila jaribu au makosa ni mkosi, bali ni hatua muhimu katika kufikia mafanikio ya
unachokiamini.
Alisema
askari huyo atakuwa ameshinda hofu, vitisho na uoga alivyosema ni miongoni mwa
dhambi kuu katika maisha ya mwanadamu na kuwataka Watanzania kutoogopa lolote,
hata ikibidi kifo wakati wakipigania haki zao kwani hakuna atakayeishi milele
kwa kuogopa kufa.
“Ni heri mtu
kuishi miaka michache duniani na Jina lake kubaki linaishi kwa haki na wema
kuliko kuishi miaka mingi akatoweka kama mzoga” alisema Lema akimkariri Mwana
mapinduzi Steve Biko na kuongeza “Ni dhambi kubwa katika demokrasia kuupuuza
ukweli eti kwa sababu anayesema uongo amejifunza kupiga na
kuua,”
Lema
aliishauri JWTZ kutekeleza ahadi ya kulinda Taifa hata kwa kukemea kwa maneno
wizi wa mali na rasilimali za umma zikiwemo fedha na wanyapori wanaotoroshwa
kwenda nje kwa msaada wa waliokabidhiwa dhamana ya kuvilinda na kuvitunza kwa
faida ya wote.
Post a Comment