Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA KUJITOLEA SERIKALI YATANGAZA KUTENGA BILIONI 1.5 KUSAIDIA VIJANA.




Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akifungua rasmi Siku ya Kimataifa ya Kujitolea bila malipo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Disemba ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Volunteer Action Counts’.

Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kujitolea Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Bi. Venerose Mtenga akihutubia na kuwaasa vijana kufanya kazi kwa kujitolea bila kusubiri malipo.

Mgeni rasmi amewaasa vijana kuwa tayari kufanya kazi kwa kujitolea kwa sababu Serikali kupitia Wizara yake imetenga Bilioni 1.5 kwenye mfuko Maalaum wa Vijana ili kuwakopesha vijana kwenye vikundi vidogo vidogo ili wajiunge na ujasiriamali na kujitoa katika umaskini.

Mshehereshaji wa Siku ya Kimataifa ya kujitolea Austin Makani akijadiliana na washiriki kuhusiana na umuhimu wa vijana kujitolea.

Kutoka kushoto ni Mgeni rasmi Bi. Venerose Mtenga, Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Bw. Phillippe Poinsot na Afisa Program wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitole (UNV) Bi. Stella Karegyesa wakifuatilia program zilizokuwa zikiendelea wakati wa maadhimisho hayo.

Pichani Juu na Chini baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali, wanachama wa UN Clubs na wageni waalikwa waliohudhuria maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kujitolea.

Baadhi ya washiriki wakijadiliana umuhimu wa kujitolea katika makundi.

Mgeni rasmi Bi. Venerose Mtenga na Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Bw. Phillippe Poinsot wakitoka ukumbi.

Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kujitolea Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Bi. Venerose Mtenga, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot na Afisa Program wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitole (UNV) Bi. Stella Karegyesa katika picha ya pamoja na washiriki.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top