Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akiwahutubia wafuasi wa chama hicho katika mkutano wa kufunga mwaka uliofanyika viwanja vya Kibandamaiti.
Mwakilishi
wa Jimbo la MjiMkongwe Zanzibar Ismail Jussa Ladhu (CUF), akiwahutubia
wafuasi wa chama hicho katika mkutano wa kufunga mwaka uliofanyika
viwanja vya Kibandamaiti.
Kaimu
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Hamad Massoud Hamad, akiwahutubia
wafuasi wa chama hicho katika mkutano wa kufunga mwaka uliofanyika
viwanja vya Kibandamaiti.
Wafuasi na wapenzi wa CUF wakiwa katika mkutano wa kufunga
mwaka ulioandaliwa na chama hicho katika viwanja vya Kibandamaiti
Na Hassan Hamad OMKR
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amesema mwaka 2012 umekuwa na umuhimu wa kipekee katika historia ya kisiasa Tanzania.
Amesema
ndani ya mwaka huu unaomalizika Watanzania katika mikoa yote wamepata
fursa ya kutoa maoni yao juu ya uundwaji wa katiba mpya ya Tanzania
ambayo yatatoa mwelekeo imara wa mustakbali wa nchi.
Maalim
Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ametoa kauli
hiyo mwishoni mwa wiki wakati akihutubia mkutano maalum wa hadhara wa
Chama hicho kwa ajili ya kuuaga mwaka 2012, uliofanyika viwanja vya
Kibandamaiti Zanzibar.
Amesema
suala la kuwashirikisha wananchi katika jambo kubwa kama hilo la kuamua
juu ya mustakbali wa nchini yao ni la kihistoria, na kutaka maoni ya
wananchi wa pande mbili za Muungano yathaminiwe na yaheshimiwe.
Amempongeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwa
kubariki uundwaji wa katiba mpya ya Tanzania na kuwashirikisha wananchi,
suala ambalo lilikosekana katika awamu zilizopita za uongozi.
“Nachukua
fursa hii kumpongeza sana Rais Kikwete kwa kubariki jambo hili, wakati
wa marehemu Mwalimu Nyerere ilionekana kama uhaini kuzungumzia masuala
ya Muungano hadharani lakini leo hii kila mwananchi anayo haki ya
kuujadili kabisa”,alieleza Maalim Seif na kuongeza kuwa hiyo ni hatua
kubwa zaidi ya kisiasa kuwahi kufikiwa Tanzania.
Ameuombea mwaka mpya wa 2013 uwe wa neema ambao utaisababishia Zanzibar kusonga mbele katika kufikia malengo yake iliyojipangia.
Maalim
Seif amewashuku wananchi wa Zanzibar kwa kuonyesha mshikamano wakati wa
utoaji wa maoni, na kwamba umoja wa Wazanzibari ndio utakaopelekea
kupatikana kwa Zanzibar yenye mamlaka kamili ndani na nje ya Zanzibar.
Kwa
upande wake Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Hamad Massoud Hamad
amesema chama chake kinajipanga kwa ajili ya kupata ushindi mkubwa
katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Amewaomba
wananchi kuendelea kukiunga mkono chama hicho ili kiweze kutatua kero
ya ukosefu wa ajira unaowakabili vijana wengi wa Zanzibar.
“Vijana
wengi wa Zanzibar bado hawana ajira, vijana hawa wamesoma wengine hadi
vyuo vikuu na wazee wao wametumia fedha nyingi kuwasomesha lakini wapi,
ajira imeota mbawa”,alisema Hamad Massoud.
Nae
Mwakilishi wa Jimbo la Mjimkongwe Ismail Jussa Ladhu, amesewa
Wazanzibar wameitumia vyema fursa yao ya kutoa maoni, tofauti na
ilivyoelezwa na baadhi ya wajumbe wa Tume wa kukusanya maoni.
Amefahamisha
kuwa maoni waliyoyatoa Wazanzibari ni sahihi na wala hawakupoteza fursa
hiyo kama ilivyodaiwa, ikizingatiwa kuwa suala la msingi kwa Zanzibar
ndani ya Muungano ni “Muungano wenyewe” kwa vile Zanzibar ina katiba
yake ambayo imeweka wazi juu ya masuala yote yanayohusu nchi ya
Zanzibar.
Post a Comment