Balozi
mdogo wa India aliyepo Zanzibar Pawan Kumar akizungumza na Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ofisini kwake
Migombani
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akimkabidhi kitabu cha urithi wa Zanzibar balozi mdogo wa India Pawan Kumar baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwake Migombani.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiagana na balozi mdogo wa India Pawan Kumar baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwake Migombani.
Balozi mdogo wa Msumbiji aliyepo Zanzibar Bw. Benuardo Constatino Lidimba akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ofisini kwake Migombani
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiagana na balozi mdogo wa Msumbiji aliyepo Zanzibar Bw. Benuardo Constatino Lidimba baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwake Migombani.(Picha na Salmin Said, OMKR).
Na Hassan Hamad OMKR

Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema serikali
inathamini sana mchango unaotolewa na serikali ya India katika kukuza
uchumi na ustawi wa wananchi wa Zanzibar.
Maalim
Seif ametoa kauli hiyo leo alipokuwa na mazungumzo na balozi mdogo wa
India aliyepo Zanzibar Bw. Pawan Kumar huko ofisini kwake Migombani.
Amesema
India imeendelea kuwa mshirika wa karibu wa Zanzibar katika kusaidia
maendeleo ya nchi hasa katika sekta za Afya na elimu.
Amefahamisha
kuwa Zanzibar imekuwa ikinufaika kikamilifu kutokana na ushirikiano wa
muda mrefu uliopo kati yake na India, na kusisitiza kuendelezwa kwa
ushirikiano huo kwa maslahi ya pande hizo mbili.
Amesifu
umakini wa watumishi wa India hasa katika sekta ya afya, sambamba na
kusifu ubora wa elimu inayotolewa nchini humo, na kwamba Zanzibar
inaweza kujifunza zaidi katika maeneo hayo.
Kwa
upande wake balozi mdogo wa India Bw. Pawan amemuhakikishia Makamu wa
Kwanza wa Rais kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Zanzibar katika
maeneo tofauti yakiwemo kutoa fursa za masomo kwa wanafunzi wa
Zanzibar.
Amefahamisha
kuwa idadi ya wanafunzi wa Zanzibar wanaosoma nchini India imekuwa
ikiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo kwa mwaka huu wa masomo jumla ya
wanafunzi 72 wamepatiwa fursa hiyo tofauti na mwaka jana ambapo walikuwa
wanafunzi 48.
Wakati
huo huo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amekutana na balozi mdogo
wa Msumbiji Bw. Benuardo Constatino Lidimba aliyefika ofini kwake kwa
ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wa utumishi hapa nchini.
Katika
mazungumzo hayo balozi Lidimba ameishauri Serikali ya Mapindizi ya
Zanzibar kuangalia uwezekano wa kukuza biashara kati ya Zanzibar na
Msumbiji, kwa kuwawezesha wafanyabiashara kuweza kufanya shughuli zao za
uhakika.
Amesema
wafanyabiashara wengi wa Zanzibar wanaofanya biashara nchini Msumbiji
wamekuwa wakibahatisha maisha yao kutokana na kutumia usafiri wa
majahazi ambao sio wa uhakika kuweza kufanyia shughuli hizo.
Kwa
upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais amesema serikali inaendelea
kulifanyia kazi tatizo hilo ambapo kwa sasa imo katika mkakati wa
kutafuta meli mpya kwa ajili ya kupata usafiri wa uhakika,
utakaowawezesha wananchi na wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwa
uhakika.
Amesema
katika kukabiliana na tatizo hilo serikali pia imekuwa ikifanya
mazungumzo na wafanyabiashara mbali mbai ili waweze kuwekeza katika
sekta ya usafiri wa baharini.
Ameongeza kuwa lengo la serikali ni kuwa na usafiri
wa kisasa na wa uhakika ambao utasaidia kuiunganisha Zanzibar na nchi
jirani, hatua ambayo itasaidia kukuza uchumi kwa haraka.
Post a Comment